tuwasiliane

Sunday, November 6, 2016

Simon Msuva Mchezaji Bora Ligi Kuu Oktoba

Simon Msuva Mchezaji Bora Ligi Kuu Oktoba
Winga wa klabu ya Yanga Simon Msuva ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba waLigi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Msuva alikuwa na washindani wa karibu wawili katika kinyang'anyiro hicho cha Oktoba ambao wote ni kutoka Simba. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya ambaye amekuwa mwiba mbaya dhidi ya timu nyingi Ligi Kuu msimu huu na Muzamiru Yassin.
Katika mwezi Oktoba ambao kulikuwa na mechi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14 huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho.
Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita cha shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ni dhahiri mchezaji huyo wa Yanga amekuwa mhimili kwa timu yake na amestahili kupata tuzo hiyo kama thawabu ya jitihada zake dimbani.

No comments:

Post a Comment