tuwasiliane

Saturday, November 5, 2016

Nicol Abwata: Liverpool haiwezi kutwaa ubingwa Klopp ni tatizo kubwa

Eti! Liverpool hawawezi kutwaa ubingwa wa Ligi kwa sababu Jurgen Klopp ndiye ‘tatizo kubwa’. Unakubaliana na kauli hii?
Nicol Abwata: Liverpool haiwezi kutwaa ubingwa Klopp ni tatizo kubwa
Je! Liverpool inaweza kutwaa ubingwa wa Ligi? Ushindani unazidi kupamba moto, lakini legendari wa Anfield Steven Nicol bado hajashawishika kama Reds wana uwezo wa kutwaa taji.
Akizungumza na ESPN Jumatatu, Nicol alieleza kutofurahishwa na mapungufu ya safu ya ulinzi wa timu ya Liverpool:
“Huwezi kutwaa ubingwa wa Ligi kwa kuwapa wapinzani magoli, na hilo ndilo linalofanywa na Liverpool. Unapotoa zawadi ya magoli kwenye wavu wako mwenyewe, ni tatizo kubwa. Sio tatizo la kimbinu, ni tatizo binafsi”.
Dhidi ya Crystal PalaceDejan Lovren alifanya makosa mawili ambayo yaliwawezesha wapinzani kufunga goli, jambo ambalo linakubaliana na hoja ya Nicol kuhusu tatizo la ulinzi kwa Liverpool kuwa ni la ‘binafsi’, si la ‘kimbinu’.
MignoletMorenoClyne na Lovren (wote ni wachezaji waliosajiliwa na Rodgers) wote wamefanya makosa yanayoigharimu timu msimu huu, lakini Matip (aliyesajiliwa na Klopp) ndiye mchezaji tbabiti, asiyefanya makosa ya mara kwa mara kwenye safu ya ulinzi ya Liverpool.
Klopp tayari ameshwatema Moreno, Sakho na Mignolet msimu huu, na Liverpool bado ingali ikitafuta mabeki kadhaa wa kati, huenda mpango wa Klopp ni kurekebisha safu yote ya ulinzi na Je! Lovren ni miongoni mwa wachezaji watakaoliwa kichwa?
Jambo moja kwa hakika: Liverpool wanahitaji kujiimarisha kiulinzi ili kuwa thabiti katika kinyang’anyiro cha taji. Baada ya mechi 10 za Ligi ya Uingereza:
*Timu MOJA tu katika kumi za juu imekuwa na rekodi mbaya kiulinzi kuliko Liverpool (Bournemouth).
*City, Spurs, Arsenal, Chelsea na United zote zina ulinzi thabiti.
*Kwa utabiri, ikiwa Liverpool itaendelea kuruhusu magoli katika mwendo huu, basi Reds watamaliza mwaka wakiwa wameruhusu magoli 50 (sawa na msimu uliopita, klabu hiyo ilipomaliza nafasi ya nane kwenye ligi).

Msimu uliopita, mashabiki kadhaa walidai kuwa Martin Skrtel alikuwa msababishi mkuu wa udhaifu katika utendaji wa safu ya ulinzi Liverpool, lakini *hakuna kitu* kilichobadilika msimu huu, na bila ya Skrtel, Moreno, Mignolet, na Sakho, bado Reds wanaruhusu magoli lukuki.

No comments:

Post a Comment