tuwasiliane

Saturday, November 5, 2016

Matokeo yale ukweli hatukuyategemea" - Kinnah Phiri

Kinnah Phiri
Kocha wa timu ya Mbeya City Mmalawi Kinnah Phiri, amesema kwake yeye Yanga ndiyo timu bora kwenye ligi ya Vodacom ukilinganisha na klabu za Simba na Azam.
 
Phiri amekiambia chanzo kimoja., pamoja na ushindi wa mabao 2-1, walioupata mbele ya mabingwa hao watetezi lakini hali ilikuwa tete kwao kutokana na mbinu za uchezaji walizokuwa nazo Yanga.
 
“Nililazimika kusimama kwa muda wote kuwatia hamasa wachezaji wangu ili kuhakikisha tunashinda mchezo huo lakini mambo yalikuwa magumu Yanga walikuwa wakitushambulia sana hata kutumia mbinu za kupoteza muda,”amesema Phiri.
 
Mmalawi huyo amesema amecheza na klabu za Azam FC, na Simba na zote amepoteza lakini mechi zao zilikuwa nyepesi ukilinganisha na ilivyokuwa ile ya Yanga. 
 
Anasema baada ya kupata bao la mapema mambo yalikuwa magumu zaidi kwao kwani wageni wao walikuja juu na kufanya mashambulizi ya kulazimisha kutafuta bao la kusawazisha lakini vijana wangu walifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti.
 
Kocha huyo amesema kwa juhudi ambazo wachezaji wake walizionyesha kwenye mchezo wa Yanga wangefanya hivyo kwenye mechi za Simba na Azam anauhakika wangepata ushindi tena wa idadi kubwa ya mabao.
 
“Sikutegemea kama tungeweza kumaliza dakika 90, kwa kuwazuia Yanga wasipate bao la kusawazisha kwasababu walitupiga presha kubwa hasa kipindi cha pili wakitafuta bao la kusawazisha,”
 
“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kucheza kwa kujitolea na kuweza kupata matokeo yale ambayo ukweli hatukuyategemea kulingana na timu tuliyocheza nayo ambao ni mabingwa na timu kubwa Tanzania,”amesema Phiri.
 
Ushindi huo umepunguza presha ya Mmalawi huyo ambaye amekalia kuti kavu baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo wa kusuasua kwenye mbio za ubingwa wa msimu huu na sasa inashika nafasi ya saba ikiwa na pointi 19.

No comments:

Post a Comment