tuwasiliane

Saturday, November 26, 2016

El Hadji Diouf amchana Steven Gerrard

Baada ya Steven Gerrard kutangaza rasmi amechana na maisha soka wachezaji wengi wametumia nafasi mbalimbali kumpa pongezi kwa maisha yake ya soka. Mashabiki wa Liverpool wengi walimshukuru kwa muda mrefu ambao amekua kiongozi wa timu yao.
screen-shot-2016-11-25-at-12-52-35-pm
Lakini kwa mchezaji mmoja Diouf amesema kwamba Gerrard alikua mtu wa kujikweza na mbaguzi. Diouf na Gerrard walikaa pamoja Anfield kwa muda wa miaka miwili ambapo Diouf alikua ana struggle ku prove.
Kwenye kitabu cha Gerrard, Diouf alizungumziwa kama mtu ambae hakujali kuhusu soka wala Liverpool. Diouf ambae kwa sasa anamiaka 35 akiongea na Tv moja huko Ufaransa alisema kwamba Gerrard ni mtu ambaya hana heshima juu yake.
“Yule jamaa sina heshima juu yake kabisa. Wakati naingia Liverpool kuna watu ambao niliambiwa sitawagusa kwa njia mbalimbali. Mimi niligusa kwa njia zote kwenye vitu mbali mbali ambavyo watu wengine hawakujaribu kufanya hata kidogo. Ndio maana kwangu mambo yakawa magumu.”
Mtangazaji akamuuliza unamzungumzia Stevie G and Jamie, Diouf akajibu,“Ndio hao hao wawili na kuhusu yeye kutaka mimi kuwa Liverpool mimi sikuenda pale kununua nyumba na kuisha pale maisha yangu yote. Nimepita, kila muda ambao alipojaribu kujifanya nyeye ni kila kitu nilimuonyesha yeye sio kitu”


No comments:

Post a Comment