tuwasiliane

Saturday, November 26, 2016

Ubaguzi wa Simba wamchosha Ajibu, sasa kutimkia Yanga

Ibrahim Ajib

Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajibu amesema yupo tayari kuhamia Yanga kipindi hiki cha dirisha dogo kutokana na uongozi wa timu yake kushindwa kumlipa mshahara wake kwa wakati.
Ajibu ameiambia Goal , tangu kumalizika kwa mzunguko wa kwanza hana furaha ndani ya timu hiyo na sababu kubwa ni uongozi kuwadharau wachezaji wazawa kwa kuchelewesha misharaha yao na kuwathamini wachezaji wa kigeni.
“Naweza kuhamia Yanga kwenye mzunguko wa pili kwa sababu wananihitaji na mimi ni mchezaji nategemea soka kuendesha maisha yangu kama wao wanakuwa na ubaguzi bora niwaachie timu yao niende kule ninapothaminiwa,” amesema Ajibu.
Mshambuliaji huyo aliyepoteza namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Joseph Omog , katika mechi za mwishoni mwa duru la kwanza amesema vipo vitu vingi ndani ya timu hiyo vinakwenda ndivyo sivyo na wahusika wa kubwa ni viongozi .
Amesema pamoja na kuanza vizuri msimu huu, lakini itakuwa ngumu kwa Simba kutwaa ubingwa msimu huu kwa sababu kwa asilimia kubwa uongozi umekuwa ukiwavunja moyo wachezaji kutokana na ubaguzi wanaoufanya kwa kuwabagua wachezaji.
“Simba ni kweli tuna timu nzuri wachezaji tulikuwa na ari kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu lakini kila tunavyokwenda viongozi wamekuwa wakituchanganya, kwa kushindwa kutupa stahiki zetu kama posho na mishahara kucheleweshwa huku taarifa za pesa kuwepo tukiwa nazo,” amesema Ajibu.
Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao matatu tangu kuanza msimu huu amesema kufanya vibaya kwa timu hiyo katika mechi mbili za mzunguko wa kwanza kumetokana na wachezaji wenzake kucheza kwa kinyongo huku wakiwa wanaida timu hiyo mshahara wa miezi miwili.
Ajibu amebakiza miezi sita kumaliza mkataba wake wa kuichezea Simba na tayari mahasimu wao Yanga wameanza kutumia madhaifu hayo kwa kumshawishi, ili aweze kuichezea timu yao kwenye mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment