Mlinzi wa kulia wa Azam FC, Shomari Kapombe, amesema hana mpango wa kurudi Simba na kuwataka viongozi wa timu hiyo inayoongoza ligi kwa sasa kusahau hilo.
Kapombe aliyepata umaarufu mkubwa akiwa na Simba amekiambia chanzo chetu kuwa, Azam ndiyo sehemu sahihi kwake hivyo haoni sababu ya kuondoka kwasababu anachotaka anapata tena kwa wakati tofauti na ilivyokuwa Simba.
“Naomba viongozi wa Simba wasahau kuhusu mimi kurudi timu yao, nina mkataba na Azam na mipango yangu ni kubaki hapa hadi nitakapo staafu kucheza soka, amesema Kapombe.
Beki huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa majeruhi amesema pamoja na kuwa na mahusiano ya karibu na viongozi wa Simba lakini anawaomba waheshimu mkataba wake na kwamba yeye kwa sasa ni mwajiriwa wa timu nyingine na wanapaswa kuwa wapole.
Kapombe amesema fikra zake kwa sasa ni kutazama namna gani anaweza kuipa mafanikio timu yake hiyo aliyojiunga nayo misimu miwili iliyopita akitokea AS Nacy ya Ufaransa ambapo alikwenda kwa ajili ya kufanya majaribio ili kuichezea tiu hiyo.
“Mimi naomba wasiumize kichwa kuhusu mimi kwasababu sina mpango wa kuondoka Azam na hivi karibuni natarajia kusaini mkataba mpya ambao utakuwa wa muda mrefu hadi 2020 kwaiyo nivyema wakatumia muda huo kutafuta mtu mwingine,” amesema Kapombe.
Mchezaji huyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amezungumzia afya yake na kusema yupo fiti na anachosubiri ni kuanza kwa mazoezi ya mzunguko wa pili ili kuungana na wenzake mazoezini.
Amesema maumivu ya goti yaliyokuwa yakimsumbua kwenye mzunguko wa kwanza yamepona na tayari ameanza mazoezi mepesi mepesi kujiandaa na mzunguko wa pili.
No comments:
Post a Comment