tuwasiliane

Monday, February 1, 2016

SIMBA YAIZIDI YANGA KWA UPELEKA WACHEZAJI NJE

Simba yaidizi Yanga kwa kutoa wachezaji wengi kwenda kucheza soka nje
Kwa muda mrefu soka la Tanzania limekuwa likitawaliwa na timu kubwa mbili ambazo ni Simba na Yanga ambazo kwa muda mrefu kabla ya ujio wa timu za Mtibwa Sugar, Mbeya City na Azam FC zenyewe ndizo zilikuwa zikipokezana ubingwa wa Ligi ya Tanzania Bara.
Rekodi zinaonyesha tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Yanga ndiyo inayoongoza kunyakua taji hilo kwa kulichukua mara 25 huku wapinzani wao Simba wakishika nafasi ya pili wakifanya hivyo mara 18.
Mbali na ushindani wa kupigania taji hilo lakini timu hizo zimekuwa na ushindani mkubwa siyo tu wa ndani ya uwanja bali hata nje ya uwanja kwa maana ya mafanikio kumiliki majengo kusajili wachezaji kwa kutumia garama kubwa ya pesa na vingine vingi.
Lakini wakati Yanga wanakuwa vinara kwa kuchukua ubingwa wa Ligi ya Tanzania mara 25 na kusifika kwa kumilikiwa na wafadhili wenye pesa nyingi na kumiliki jingo zuri timu hiyo bado haijaweza kuwafikia Simba kwa kutoa idadi kubwa ya wachezaji kwenda kucheza soka nje ya nchi.
Simba ndiyo timu pekee Tanzania inayoongoza kwa kuuza wachezaji wake kwenda kucheza soka barani Ulaya na hata timu kubwa zinazofanya vizuri Afrika huku Yanga wao wakifuatia kufanya hivyo huku sababu kubwa ikidaiwa kuwa timu hiyo imekuwa na utaratibu mbovu wa kuwazuia wachezaji wake kwenda kucheza nje.
Ukimtoa mshambuliaji Nonda Shaban ‘Papii’ aliyechezea Yanga kwa kipindi kifupi na baadaye kutimkia Afrika Kusini na kisha kujiunga na Manaco ya Ufaransa alipopata umaarufu mkubwa kutokana na kufanya vizuri na kusababisha kuwania na timu kubwa zaidi za AC Millan, Lazio Inter Millan na hata Manchester United na FC Barcelona ya Uingereza hakuna mchezaji mwengine
ambaye alipita Yanga na kwenda nje.

Edibili Lunyamila Winga machachari aliyetingisha Afrika Mashariki na Kati kutokana na uwezo aliokuwa nao mwaka 1995, alipata nafasi ya kwenda Ujerumani kucheza soka la kulipwa akitokea Yanga lakini viongozi wa timu hiyo walimkatili kwa kumrudisha Taanzania akiwa kwenye majaribio yaliyokuwa yanaelekea kufanikiwa kwa ajili ya kuja kucheza na Simba kwenye mechi ya Kombe la Hedex.
Baada ya Lunyamila likafuata kundi kubwa la wachezaji ambao kiliwatokea kilichomkuta mkongwe huyo kama vile Jeryson Tegete msimu wa 2009,2010 aliporudishwa Tanzania akitokea Sweden kwenye majaribio aliyokuwa anaelekea kufanikiwa .
Baada ya kueleza namna ambavyo Yanga ilivyoshindwa na wapinzani wao katika mafanikio ya kuuza wachezaji nje ya Tanzania Mtandao wa Goal unakuletea baadhi ya wachezaji walicheza Simba na kuuzwa kwenye timu za nje ya Tanzania na wakafanya vizuri.
1.Renatus Njohole alijiunga na Simba mwaka 1999 akitokea Mirambo ya Tabora na alicheza kwa misimu mitatu kabla ya mwaka 2014 kuuzwa nchini Switzerland kwenye klabu ya Yverdon Sports alipocheza kwa msimu mmoja na msimu wa 2005 alifanya vizuri na kuivutia klabu ya FC Valmountaliyoichezea kwa misimu miwili kabla ya kuhamia timu ya FC Le Mont ambayo nayo aliichezea kwa misimu miwili kabla ya msimu wa 2010 kujiunga na klabu ya Bavois aliyostaafia.
Uhamisho huu uliiwezesha Simba kupata kiasi kikubwa cha pesa ambazo ziliwasaidia kufanya usajili mzuri kwa kusajili wachezaji wengine kuziba pengo la Njohole.
2.Mbwana Samatta Huyu ni mshambuliaji wa zamani wa  TP Mazembe ya DR Congo ambaye kwa sasa amesajiliwa na Genk ya Ubelgiji baada ya kuwa na mwaka wa kipekee kwa mwaka 2015 akiumaliza kwa kutwaa Tuzo ya mchezaji bora Afrika, ni mchezaji mwenye mafanikio zaidi kutoka Tanzania kwa sasa

3.Patrick Ochang kiungo huyu mshambuliaji raia wa Uganda naye aliongozana na Samatta mwaka mmoja kujiunga na TP Mazembe kwa ada kama hiyo ya dola 100,000 na hiyo ni kutokana na kuwavutia mabingwa hao mara mbili wa Afrika ambao lakini yeye hakuweza kufanyavizuri baadaye alitemwa na kumuacha Samatta.
4.Seleman Matola aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba akimsaidia kocha muingereza Dylan Kerr, alikuwa ni mmoja wa viungo hodari waliopata kutokea kwa taifa la Tanzania na alikuwa na mchango mkubwa kwenye klabu ya Simba na kuzivutia timu nyingi na kubwa Afrika lakini Super Sport ya Afrika Kusini akafanikiwa kumnunua baada ya kocha wake wa wakati huo Pitso Mosimane,
Haikujulikana nyota huyo alinunuliwa kwa kiasi gani cha pesa lakini rekodi pekee aliyoiweka katika usajili wake ni kujiunga moja kwa moja na klabu hiyo pasipo kufanya usajili kama ilivyokuwa kwa Samatta na Ochan.
5.Haruna Moshi ‘Boban’ Kiungo mtukutu huyo ambaye anakiwango kikubwa cha soka ameweza kuitumikia Simba kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuuzwa nchini Sweden kwenye klabu ya Gefle FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo tena kwa kiasi kikubwa cha pesa.
Ingawa nyota huyo hakudumu sana na timu hiyo baada ya kuvunja mkataba kutokana na madai ya kutopata maslahi lakini Simba ndiyo iliyomtoa hadi kumfikisha kwenye hatua ya kucheza soka la kimataif.
6.Henry joseph Kiungo huyo naye alitamba na Simba na baadaye mwaka 2006 aliuzwa Kongsvinger FC,inayoshiriki Ligi Kuu nchini Norway na alicheza kwa mafanikio katika kipindi cha miaka minne na baada ya hapo alirudi nyumbani na kuendelea kuichezea Simba
Japo safari hii hakuweza kudumu kutokana na kiwango na umri wake kumtupa mkono na msimu uliomalizika aliweza kuwekwa pembeni na nafasi yake kuchukuliwa na vijana Jonas Mkude na Said Ndemla.
7.Athuman Machupa Nyota mwingine ambaye alipata nafasi ya kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Vasalund IF ya Sweden ,akitokea Simba ya Tanzania ambayo ilimuuza huko baada ya kungara akiwa na mabingwa hao wa zamani wa Tanzania.
Simba ilimuuza machupa Sweden baada ya mchezaji huyo kufanya vizuri kwa kuiwezesha timu hiyo kunyakua ubingwa wa Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi 2004 mafanikio hayo akiwa na Simba yalimsaidia kuonekana na kupata timu hiyo iliyomnunu bila ajizi.
8. Eme Ezechukwu. mshambuliaji huyo,raia wa Nigeria naye alitamba na Simba na baadaye mwaka 2006 aliuzwa Kongsvinger FC,inayoshiriki Ligi Kuu nchini Norway na alicheza kwa mafanikio 

No comments:

Post a Comment