tuwasiliane

Saturday, January 30, 2016

RASMI SAMATTA ATUA KRC GENK

Mara baada ya Mbwana Samatta kukamilisha taratibu zote za kujiunga na klabu ya Genk, nyota huyo wa kwanza kutoka Bongo kwenda kucheza professional soccer barani Ulaya aliongea mbele ya waandishi wa habari akieleza anavyojisikia mara baada ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu hiyo.
Samatta amesema alikuwa anahisi anakuwa chizi kutokana na furaha aliyokuwa nayo baada ya dili hilo kukamilika ambalo limeifanya ndoto yake ya siku nyingi ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya kukamilika.
“Nilikuwa nahisi nakuwa chizi kutokana na furaha niliyokuwa nayo. Ukiwa na ndoto halafu unaona ndoto yako inakuwa kweli, na kilichotokea ni kama kuna giza mbele na unashindwa kuona hicho ndicho kilichotokea kwangu”, alisema Samatta.
“Naiheshimu TP Mazembe, namuheshimu Rais wa Mazembe Moise Katumbi. Sitaki kusababisha matatizo yoyote na wao kwasababu wamenichukua tangu nikiwa mdogo na kunilea. Nimekulia Mazembe nikisubiri wakati muafaka hadi klabu yangu ifikie makubaliano na klabu inayonihitaji”.
Samatta amesaini kandarasi ya miaka minne (4) kukitumikia kikosi cha Genk ambapo anatarajia kuhudumu kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment