Baada ya kufanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika inayotolewa na Shirikisho la soka Afrika CAF, mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta amesema yupo tayari kuununua mkataba wake uliobaki na TP Mazembe ili ajkajiunge na timu ya Genk ya Ubelgiji ambayo tayari ameshasaini nayo mkataba wa awali.
Mshambuliaji huyo bora wa Mtandao wa Goal mwaka jana ameuambia mtandao huu kuwa anataka kufanya hivyo kwasababu Mmiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi, ambaye anataka mchezaji huyo aendelee kuitumikia timu hiyo ambayo ni Mabingwa wa Afrika.
“Nimezungumza na Meneja wangu Jamal Kisongo, na kwapamoja tumekubaliana kuununa mkataba ili niweze kupata nafasi ya kujiunga na Genk, kwavile naamini kucheza kule itakuwa karibu kuonekana na kujiunga na timu kubwa za Ulaya.
Mkataba wa Samatta na Mazembe unamalizika Aprili 2016, na Katumbi anataka kumzuia mshambuliaji huyo abaki kuichezea timu hiyo kitu ambacho mwenye hakipendi.
Samatta ameibuka mshindi kwenye tuzo hiyo akipata kura 127, huku mchezaji mwenzake kipa wa TP Mazembe Robert Kidiaba akipata kura 86 na Mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad akishika nafasi ya tatu na kuambulia kura 63.
No comments:
Post a Comment