Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ limesema michuano ya Kombe la Kagame kwa mwaka 2016, itafanyika Julai na Agosti mwaka huu Visiwani Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CACAFA, Nicholaus Musonye ameiambia Goal, leo kuwa sababu ya kuipeleka michuano hiyo huko ni kutokana na wakazi wa visiwani humo kukosa kuishuhudia kwa muda mrefu ikifanyika kwenye ardhi ya kwao.
“Tunafuraha kuona Zanzibar wanapata nafasi ya kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Kagame kwa mwaka huu, baada ya muda mrefu kupita naamini hiyo ndiyo furasa pekee kwa klabu na wadau wa soko Visiwani humo kuweza kushuhudia live michuano ya mwaka huu ikifanyika nchini kwao,”amesema Musonye.
Vinara wa Ligi ya Vodacom Tanzania Azam FC ndiyo wanashikilia taji hilo baada ya kulinyakua msimu uliopita kwa kuifunga Gor Mahia ya Kenya kwenye mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment