tuwasiliane

Friday, January 8, 2016

Choo kinachojifungua na kujiosha

Choo
Choo cha kisasa ambacho kina uwezo wa kujifungua unapokaribia na pia kujiosha, ni moja ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya teknolojia mpya za bidhaa za elektroniki Las Vegas.
Choo hicho, kilichopewa jina Neorest, pia humsafisha anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa mtu akiwa ameketi.
Kina pia teknolojia inayokiwezesha kuua bakteria na virusi.
Licha ya choo hicho kuuzwa $9,800 (£6,704), waliotengeneza choo hicho vyoo zaidi ya 40 milioni vya miundo ya awali vimeuzwa.
Kampuni ya Toto, iliyotengeneza choo hicho, imesema muundo huo wa sasa bado unaendelea kuboreshwa.
"Huhitaji kuosha bakuli la choo kwa kipindi cha mwaka mmoja,” anasema msemaji wa Toto, Bi Lenora Campos.Choo hicho hata hivyo si kwamba kitakuondolea kabisa majukumu yote ya usafi chooni, kwani hakiwezi kujiosha upande wa nje iwapo kutakuwa na uchafu.

Maonyesho hayo ambayo kwa Kiingereza yanajulikana kama Consumer Electronics Show hufanyika kila mwaka ambapo kampuni mbalimbali na wavumbuzi huonyesha teknolojia za karibuni zaidi.
source bbc

No comments:

Post a Comment