tuwasiliane

Wednesday, January 13, 2016

KERR ATIMULIWA SIMBA SPORTS CLUB

Kerr akisalimiana na kocha mpya msaidizi Jackson Mayanja
Uongozi wa klabu ya Simba umemfukuza kazi kocha wake mkuu Muingereza Dylan Kerr, kuanzia jana Januari 12
Sababu kubwa ikiwa ni timu hiyo kufanya vibaya kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi abaada ya kutolewa hatua ya nusu fainali na Mtibwa Sugar.
Rais wa Simba Evans Aveva amekiambia chanzo chetu, maamuzi hayo yamepitishwa na kikoa cha dharura kilichokaliwa usiku wa kuamkia leo na kupitia mambo mbalimbali ikiwemo mwenendo wa timu yao katika Ligi ya Vodacom na ushiriki wake katika Kombe la Mapinduzi na kugundua kocha ndiyo tatizo na kupitisha maamuzi ya pamoja kusimamisha mkataba wake.
“Ni maamuzi ya kawada wala siyo mageni na yana lengo zuri la kuinusuru timu yetu kwa sababu tunapoelekea siyo kuzuri ndiyo sababu Kamati ya utendaji ikaamua kuchukua uamuzi huo ambao nadhani umekuja wakati muafaka katika harakati zetu za kupigania ubingwa wa Tanzania bara msimu huu," amesema Aveva.
Aveva amesema tayari wamemwita kocha huyo kutoka Zanzibar na kumpa ukweli juu ya taarifa hizo za kusitisha mkataba wake na kwasasa wapo katika hatua za mwisho kumalizana kwa kumpa stahiki zake ili aweze kuondoka nchini kurudi kwao Uingereza.
“Baada ya kumalizana naye tumeanza mchakato wa kumpata kocha mpya atakaye chukua nafasi ya Kerr lakini kwa sasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Jackson Mayanja ambaye anasiku chache tangu achukuliwe na timu hiyo akitokea Coastal Union ya Tanga.
Kerr anaondoka na kuiacha Simba katika nafasi ya tatu baada ya mechi 13 na imekusanya pointi 27 nyuma ya Yanga yenye 33 na Azam FC kileleni ikiwa na 35.
Baada ya taarifa hizo katika mitandao y ya kijamii Kerr, amewashuku mashabiki na wachezaji wa timu hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo miezi sita iliyopita.
Katika kipindi cha miezi sita aliyoifundisha timu hiyo ameiongoza kushinda mechi 8, sare 3 na kupoteza mbili, imefunga mabao 20 ikishika nafasi ya tatu kwa ufungaji baada ya Yanga yenye 30 na Azam FC yenye 27 huku ikiwa imeruhusu mabao 9, ikiwa safu bora ya ulinzi katika nafasi ya nne baada ya Azam iliyoruhusu mabao 8, Mtibwa Sugar mabao 7 na Yanga yenye safu ngumu zaidi imefungwa mabao matano.

No comments:

Post a Comment