tuwasiliane

Saturday, January 2, 2016

EXCLUSIVE: TP MAZEMBE YAPOKE OFFER RASMI KUTOKA KLABU YA ULAYA IKIMTAKA THOMAS ULIMWENGU

Thomas Ulimwegu wa TP Mazembe akiachia shuti
Neema imezidi kuwashukia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania wanaokipiga kwenye klabu ya TP Mazembe ya Congo DR. Baada ya Mbwana Samatta kupata timu ya barani Ulaya hatimaye pacha wake Thomas Ulimwengu ‘Drogba wa Dodoma’ naye huenda akaungana na Samatta kwenda kuchea soka la kulipwa barani Ulaya.
Klabu ya TP mazembe imethibitisha kupokea offer rasmi kutoka timu ya AS Saint-Étienne inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1.
TP Mazembe iko tayari kumwachia Ulimwengu kwenda kukipiga nchini Ufaransa kutokana na kuondoka kwa ‘pacha wake’ Mbwana Samatta ambaye yeye (Samatta) anaelekea nchini Ubelgiji kujiunga na klabu ya Genk ambayo inashiriki ligi kuu nchini humo inayofahamika kwa jina la Belgian Pro League.
Uongozi wa Mazembe umesema hauna tatizo juu ya suala hilo na uko tayari kumwachia Ulimwengu aondoke kwasababu hatakuwa katika wakati mzuri hasa kutokana na upweke unaotokana na kuondoka kwa Mbwana Samatta kwenye klabu hiyo.
Samatta na Ulimwengu wamekuwa karibu sana ndani na nje ya uwanja kwa muda wote ambao wamekuwa wakiitumikia klabu ya Mazembe, kuondoka kwa Samatta kwenye kikosi cha Mazembe huenda kukamfanya Ulimwengu awe mpweke (bored), ili hali hiyo isimkute Ulimwengu Mazembe wanaona ni vyema kumruhusu aondoke kwenda kwenye klabu mpya ambapo atakutana na changamoto mpya.
AS Saint-Étienne ipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligue 1 ikiwa imecheza mechi 19 na kukusanya pointi 29 hadi sasa. Imeshinda mechi tisa, imetoka sare michezo miwili na kupoteza mechi nane.
Hizo ni habari nzuri kwa Thomas Ulimwengu na kwa watanzania wote kwa ujumla, kufanikiwa kwa nyota hao kwenda kucheza soka barani Ulaya kutafungua fursa kwa wacheaji wengine wa kitanzania kwenda Ulaya lakini kutaisaidia timu ya taifa ya Tanzania kutokana na uzoefu watakaoupata kwenye timu zao za Ulaya ambapo tunaamini wao wamepiga hatua kwenye soka.
source shaffihdauda

No comments:

Post a Comment