tuwasiliane

Saturday, January 2, 2016

EXCLUSIVE: CHANONGO, UBWA, WATUA TP MAZEMBE

Haruna Chanongo (kulia) Abuu Ubwa (kushoto) na mjumbe wa kamati kuu ya klabu ya TP Mazembe Frederic Kitengie
Wachezaji wawili wa kitanzania Haruna Chanongo na Abuu Ubwa wote kutoka Stand United ya mkoani Shinyanga, wamesafiri leo asubuhi kuelea nchini Congo DR kufanya majaribio kwenye klabu ya TP Mazembe kwa ajili ya kuziba nafasi ambazo zitaachwa wazi na watanzania wanaokipiga kwenye klabu hiyo ambayo ndiyo mabingwa wa taji la vilabu bingwa Afrika.
Frederic Kitengie mjumbe wa kamati kuu ya TP Mazembe amesafiri na wachezaji hao kuelekea Congo kwa ajili ya majaribio na endapo watafanikiwa kufuzu majaribio watajiunga na kikosi cha miamba hiyo ya bara la Afrika.
Barua ya mwaliko kutoka TP Mazembe ikiwaalika Haruna Chanongo na Abuu Ubwa kwenda kwenye klabu hiyo kwa majaribio
Mchezaji wa Mtibwa Sugar Mohamed Ibrahim pia ilibidi asafiri leo pamoja na Chanongo, na Ubwa kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio Mazembe lakini wakati anatafutwa mara nyingi simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani na ilipopaikana haikujibiwa.
Wachezaji wengine ambao walikuwa kwenye ‘radar’ ya TP Mazembe ni pamoja na Kipre Tchetche wa Azam FC pamoja na Amis Tambwe wa Yanga lakini uongozi wa Mazembe uliahirisha mpango wa kwanasa wachezaji hao kutokana na umri wao kuwatupa mkono. Baada ya kupiga chini dili la kuwanasa wakongwe hao, sasa radar ya TP Mazembe imehamia kwa Ibrahim Ajib wa Simba SC na Elius Maguli wa Stand United.
Mazembe wanahitaji wachezaji vijana zaidi kwasababu inaamini wanauwezo wa kukaa na kujifunza na kuzoea mazingira pamoja na kupata uzoefu wa kutosha kabla ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza na kuanza kufanya vyema.
Mwaka 2011 Mbwana Samatta na Patrick Ochang walisajiliwa na TP Mazembe wakitokea klabu ya Simba, Ochang licha ya kuwa kwenye kiwango cha juu alihitaji muda kwenye kikosi cha Mazembe lakini kwa vile alikuwa na umri mkubwa ilikuwa ni vigumu kwake kukaa nje kwa zaidi ya miaka miwili tofauti na Mbwana Samatta ambaye alikaa na kujifunza na kupata uzoefu hatimaye kufanya vizuri kwasababu umri wake ulimruhusu kufanya hivyo.
Jopo la ‘ma-scout’ kutoka TP Mazembe limekuwepo nchini likifatilia wachezaji kuona wale ambao wanaweza wakawa na uwezo wa kucheza kwenye klabu yao.
Uongozi wa Mazembe unatafuta wachezaji wa kitanzania kutokana na kiwango cha juu kilichooneshwa na Samatta na Ulimwengu ambao wamekuwa ‘dhahabu’ kwenye kikosi cha TP Mazembe na kujenga imani kubwa kwa uongozi wa timu yao juu ya wachezaji wa Kitanzania.
source shaffihdauda

No comments:

Post a Comment