tuwasiliane

Sunday, January 3, 2016

Carragher;Bado Mesut Ozil hajawa Mshindi

Mesut Ozil
Jamie Carragher ameibua hoja mpya, adai kuwa pasi nyingi za mabao za Mesut Ozil zitakuwa si kitu iwapo Arsenal itashindwa kunyanyua taji la Ligi ya Uingereza mwezi Mei.
Mjerumani huyo ametajwa kuwa mchezaji wa Arsenal aliyefanya kazi kubwa msimu huu, baada ya kufikisha pasi 16 zilizozaa magoli, ni tishio sasa kwani anakaribia kuvunja rekodi ya Thierry Henry ya pasi 20.
Hata hivyo, nahodha wa zamani wa Liverpool, Carragher amesisitiza kuwa vijana hao wa Arsene Wenger wanahitaji kushinda taji kubwa la Uingereza ili kuifanya kazi nzuri ya Ozil ionekane kuwa na tija.
Gwiji huyo wa Liverpool alikiambia Daily Mail "Hesabu zake zinaonekana. Anaelekea kuvunja rekodi lakini kama hatapata medali, itakuwa na maana gani?"
"Unamkumbuka Thierry Henry kwa magoli na mataji au kwa sababu aliweka rekodi ya pasi nyingi za mwisho (20) msimu wa 2002/03?"
Washika Mtutu wamejitwalia Kombe la FA mfululizo tangu ujio wa Ozil mnamo 2013, Lakini Arsena ina changamoto kubwa ya kuusaka ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza ambao waliutwaa kwa mara ya mwisho 2004.

No comments:

Post a Comment