Kocha wa vinara wa Ligi ya Vodacom Tanzania Azam FC, Stewart Hall, amesema wanakwenda kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa lengo la kubeba taji hilo.
Kocha huyo anayependa kwenda kwa mahesabu amesema wanajiamini lakini anatambua kuwa wanatakiwa kufanya kazi kubwa kutokana na ugumu wa kundi walilopanwa ambalo lina timu ngumu.
Hall amkeiambia chanzo chetu kuwa, kutokana na ugumu huo ameamua kwenda na kikosi kamili ambacho anaamini kitaweza kumudu ushindani ulipo kwenye hatua ya kundi lao B, na kuweza kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
“Mwaka huu tutakuwa na kazi kubwa ya kufanya kuanzia kwenye makundi kwani tumepangwa kundi B, na timu ngumu za Yanga, Mtibwa Sugar na Mafunzo timu ambazo tunapambana nazo kwa karibu kwenye mbio za uongozi wa ligi ya Vodacom hiki kinatulazimu kupambana ili kuonyesha ubora wetu unaotufanya tuongoze ligi kuu,”amesema Hall.
Kocha huyo amesema anachotaka ni kuona Azam inarudi na ubingwa wa michuano hiyo kutokana na kuwa na kikosi bora ambacho kinastaili licha ya changamoto ambazo watazipata kutoka kwa Azam na Mtibwa ambazo amedai wataweza kuzivuka.
Azam itafungua michuano hiyo Jumapili Januari 3 kwa kupambana na Mtibwa Sugar, mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na timu hizo kupambana jana Jumatano kwenye mechi ya ligi ya Vodacom na Azam kupata ushindi wa tabu wa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment