tuwasiliane

Sunday, December 27, 2015

YANGA ILIPOJIIMARISHA KILELENI HAPO JANA,LEO NI ZAM YA AZAM FC VS KAGERA SUGAR

Yanga SC.
Mshambuliaji Amissi Tambwe jana alifunga bao lake la 10 baada ya kufunga mabao mawili wakati yanga ikiiangusha Mbeya City kwa mabao 3-0.
Tambwe aliyekuwa mfungaji bora kabla ya msimu uliopita, amefunga mabao hayo mawili na kufikisha 10, akimvuka Elius Maguri wa Stand United aliyekuwa na mabao 9.

Kabla ya mechi hii, Tambwe alifunga mabao matatu, hat trick wakati Yanga ikiitwanga Stand United kwa mabao 4-0.
Yanga SC imetanua mbawa kileleni mwa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 33, baada ya kucheza mechi 13, wakati Azam FC iliyocheza mechi 12, ina pointi 29.
Mrundi Amissi Tambwe aliifungia Yanga SC mabao mawili mfululizo, la kwanza dakika la 37 akimalizia pasi ya winga Simon Msuva na la pili dakika ya 65 akimalizia krosi ya Mwinyi Hajji Mngwali, kabla ya kumpasia kwa kichwa Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tatu dakika ya 66.
katika mchezo mwingine wa ligi hiyo jana, Simba SC ililazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC ya kocha Jamhuri KIhwelo ‘Julio ’Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mwadui walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Nizar Khalfan dakika ya 77, kabla ya Brian Majwega kuisawazishia Simba SC dakika ya 86.leo Azam fc itacheza na kagera sugara katika uwanja wa Azam complex chamanzi wakati Toto african watawakaribisha African Sports ya Tanga Katika uwanja wa Ccm kirumba mwanza 

No comments:

Post a Comment