tuwasiliane

Saturday, December 26, 2015

MASHALI AMBUTUA CHEKA KWAO,AMPIGA KWA POINT


BONDIA Thomas Mashali kutoka Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo alimaliza ufalme wa Francis Cheka wa Morogoro baada ya kumtwanga kwa pointi kwenye pambano lao lililopigwa kwenye dimba la Jamhuri mjini Morogoro.Katika pambano la raundi 10, kila bondia alionyesha uimara katika kurusha na kukwepa ngumi huku kila mmoja akikataa kunyoosha mikono juu na kumpa mwenzake ushindi wa 'knock out'.

Mashali na Cheka wamekuwa wakitambiana kwa takribani mwezi mzima wa maandalizi lakini ubishi wa nani mbabe ulimalizwa baada ya majaji kumpa pointi nyingi zaidi Mashali.Katika mapambano ya utangulizi, bondia wa kike Lulu Kayage alimtwanga Mwanne Haji kwa pointi kwenye pambano lao la raundi 10 huku Vicent Mbilinyi nae akimshinda Deo Njiku kwa pointi kwenye pambano la raundi sita.

No comments:

Post a Comment