tuwasiliane

Tuesday, December 22, 2015

Wenger: Ushindi dhidi ya City umetupa tumaini

Meneja wa Arsenal Arsene wenger amefichua kuwa ushindi dhidi ya Man city imepiga jeki imani wanayohitaji katika mbio za kutwaa ligi ya Uingereza msimu huu.
Arsenal haijawahi kunyanyua taji hilo tangu mwaka wa 2004.
Hata hivyo mabao ya Theo Walcott na Olivier Giroud yalitosha dhidi ya Man City.
The Gunners walijifurukuta na kuwanyamazisha City mbele ya mashabiki wa nyumbani .Licha ya bao la Yaya Toure Man city hawakuweza kuizima Gunners ambao walikuwa wakitafuta alama tatu muhimu na kupunguza pengo la alama kutoka kwa vinara wa ligi hiyo Leicester.
"Inatupa ujasiri, nguvu na," alisema Wenger, mwenye umri wa miaka 66.
"Kikosi kimeonyesha ukomavu ambao ungeweza kushuhudia katika mchuano tulipokuwa na shinikizo la kufanya vyema."
Arsenal inaoongoza city kwa alama 4 lakini bado wako alama mbili chini ya vinara Leicester City.
Huku mabingwa watetezi, Chelsea wakiwa nje ya mbio za kuwania taji la ligi, mababe hao wa kusini mwa London ndio wanaopigiwa upatu kuibuka washindi wa ligi.
Arsenal haijapoteza mechi 6 na ushidi wao katika mechi tano kati ya mechi zake sita umewawezesha kuchupa hadi nafasi ya pili msimu wa krismasi."Miaka miwili au mitatu iliyopita, tuliongoza kwa kipindi kirefu lakini uzuri wa wakati huu ni kuwa tumepoteza wachezaji bora, tulicheza dhidi ya Olympiakos, Villa na leo, tumeshinda mechi zote," alisema Wenger.
"Ni ishara nzuri. Naamini tumeonyesha uwezo wetu, matayarisho, na uhodari kwa jumla na imetupa alama tatu.
"Wakati tulikuwa tumechoka tulitegemea matumaini na hilo limetuwezesha tumalize katika nafasi nzuri."
Harakati za dakika za mwisho za City zilizoongozwa na Toure hazikutosha kuilemaza Arsenal.
City walionekana kupungukiwa ushupavu wao ugani Emirates bila beki wao wa kutegemewa, Vincent Kompany na Sergio Aguero aliyepata afueni baada ya kuuguza jeraha."Ilikuwa muhimu kwa Sergio kurudi kwa timu ,labda anahitaji mechi kadhaa kurejea katika fomu yake," alidai Pellegrini.
"Kuna alama 63 za kushindaniwa , mechi kadhaa na tulivyocheza katka kipindi cha pili inaonyesha tunazidi kushindania ligi."
City wamepoteza mechi tano msimu huu na timu ya mwisho kupoteza mechi tano kabla ya Krismasi na kushinda ligi ilikuwa Everton kati ya mwaka wa 1986-87.
Hata hivyo Pellegrini amesema kuwa; "Sijui takwimu lakini hatuko nje ya mbio za kushinda ligi. Ikiwa hauamini , hauko katika taaluma."

No comments:

Post a Comment