tuwasiliane

Tuesday, December 22, 2015

KAMUSOKO ATAMANI KUTUPIA KILA MECHI

Thabani Kamusoko Yanga
Kiungo mkabaji wa Yanga, Thabani Kamusoko amesema angependa kuendelea kufunga mabao zaidi ikiwezekana kila mechi.
Kamusoko ambaye amefunga mabao mawili katika mechi mbili, amesema angependa kufunga zaidi kwa ajili ya timu lakini kwake pia.
“Kufunga ni jambo zuri sana, unakuwa umetoa msaada kwa timu. Lakini inakupa moyo kwa kuwa unapofunga unajisikia vizuri.
“Kama nitafunga kila mechi, pia litakuwa jambo zuri zaidi lakini bado ningependa kuisaidia timu pamoja na wenzangu ili tuwe mabingwa,” alisema.
Kamusoko alifunga katika mechi dhidi ya African Sports na bao lake likaweka rekodi ya kuwa bao zuri la dakika za mwisho zaidi.
Lakini jana akafunga tena bao la nne wakati Yanga ilipoishindilia Stand United kwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi zote mbili, Kocha Hans van der Pluijm amekuwa akimtumia kama kiungo mchezeshaji yaani namba 8 badala ya mkabaji.

No comments:

Post a Comment