tuwasiliane

Tuesday, December 22, 2015

Danny Lyanga;Najivunia kuwa mchezaji wa simba

Danny Lyanga Simba
Mshambuliaji wa Simba Danny Lyanga amesema ana matumaini ya kufanya vizuri msimu huu na kuipa mafanikio timu hiyo aliyoanza kuichezea baada ya kufungwa kwa dirisha dogo.
Lyanga amekiambia chanzo chetu, anajivunia kuwemo katika kikosi cha kocha Dylan Kerr na amejipanga kuonyesha kiwango chake chote kuhakikisha timu hiyo inapata mafanikio makubwa.
“Najua ligi ya Vodacom ningumu lakini kama mchezaji nimejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri na kubeba ubingwa wa Tanzania nahilo linawezekana kutokana na timu yetu kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.
Lynaga aliyefunga bao moja katika sare ya 1-1, dhidi ya Toto Africans ya Mwanza Jumamosi iliyopita amewataka mashabiki wa timu hiyo kumwamini ili aweze kutimiza ndoto zake za kuipa Simba mafanikio msimu huu.

No comments:

Post a Comment