tuwasiliane

Tuesday, December 22, 2015

Zamalek kujiondoa katika ligi ya Misri

Klabu maarufu sana ya soka nchini Misri imesema kuwa itajiondoa kwenye ligi kuu ya nchini hiyo kutokana na usimamizi mbaya wa mechi.
Klabu ya Zamaleck iliyotwaa ubingwa wa msimu uliopita ilitoa tangazo hilo baada ya kushindwa katika mechi ya jana.
Baraza kuu la klabu hiyo ilikutana baada ya kushindwa mabao 3-2 na klabu ya El-Gaish jumapili usiku na kuamua kutoendelea kutetea taji lao.
Aidha Baraza hilo linatarajiwa kukutana tena jumatatu kujadili jambo hilo.
Shirika la kandanda la Misri limesema halijapokea mawasiliano rasmi kutoka Zamalek.
Pia limetetea vikali viwango vya waamuzi wa ligi hiyo.
Kabla ya mechi hiyo dhidi ya El-Ghaish, Zamalek iliomba refarii Mahmoud Al Banna kubadilishwa kama muamuzi wa mechi lakini ombi hilo lilitupiliwa mbali.
Al Banna alimwonyesha kadi nyekundu mlinzi wa Zamalek Ali Gabr baada ya dakika nne tu na kuwapa El-Gaish penalti.
Refarii huyo aliwatunuku El-Ghaish penalti nyingine katika dakika ya 55.
Kwa mujibu wa sheria za ligi ya Misri, Zamalek wanaweza kuadhabiwa vikali na hata kushushwa daraja ya nne ya ligi wasipobadilisha uamuzi wao.

No comments:

Post a Comment