tuwasiliane

Tuesday, December 22, 2015

Hans van der Pluijm: "Mechi ya Yanga dhidi ya Stand United ilikuwa ngumu mno"

Hans van der Pluijm | Kocha wa Yanga

Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm amekiri kuwa kikosi cha Stand ni bora licha ya kufanikiwa kuwafunga 4-0.
Baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi wa mabao 4-0, mbele ya Stand United kocha wa Yanga Mholanzi Hans van der Pluijm, amesema mechi hiyo kwake ndiyo bora kuwahi kuishuhudia tangu kuanza msimu huu.
Mdachi huyo amekiambia chanzo chetu cha habari kuwa, Stand United waliwapa wakati mgumu mwanzoni mwa mchezo kiasi cha kumpa presha lakini amewapongeza wachezaji wake kwa kutumia vizuri uzoefu na mbinu alizowapa kupata ushindi huo ambao umeendelea kuwaweka kileleni mwa msimamo wa ligi ya Vodacom,  wakiwa na pointi 30.
“Ni mchezo mzuri na mgumu kwa timu zote mbili sijapata kuona kiwango bora kilichoonyeshwa na timu zote mbili msimu huu kama mchezo ule lakini nawapongeza wapinzani wetu Stand United, walicheza vizuri lakini uzoefu wa wachezaji wangu na mbinu bora ninazowapa ndizo zilizotupa matoke ya ushindi,”amesema Pluijm.
Pluijm amesema atahakikisha mbali na kupata ushindi lakini timu yake inacheza vizuri na kuonyesha burudani kwa mashabiki wao ambao wamelipa pesa zao kwa ajili ya kupata furaha kutoka kwao.

No comments:

Post a Comment