Mohamed Huessein Simba
Beki wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amebeba tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba, kwa klabu yake na kuzawadiwa na uongozi wa timu hiyo Tsh. 500,000.
Msemaji wa Simba Hajji Manara amekiambia chanzo chetu cha habari kuwa, huo ni utaratibu wao ambao wamejiwekea kwa lengo la kuongeza morali na ushindani kwa wachezaji kuzidi kujituma na kuipa timu mafanikio ambayo ndiyo lengo kubwa kwao.
“Wanachama ambao ndiyo wanaopiga kura kumchagua mchezaji bora wa kila mwezi wamemchagua Tshabalala, kutokana na mchango wake ndani ya Simba na siye kama viongozi tumekubali mapendekezo yao kwasababu kazi inaonekana hadharani na kweli anastaili,”amesema Manara.
Manara amesema wakiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma zaidi wanatambuliwa na kuenziwa.