tuwasiliane

Wednesday, December 30, 2015

Man City, Leicester City zatoka suluhu

Ligi kuu ya England iliendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa mchezo kuchezwa.
Leicester City walikua wenyeji wa Manchester City mchezo uliochezwa katika dimba la King Power na kushuhudia timu hizi mbili zikitosha nguvu kwa kwenda sare ya bila kufungana.
Man City ndio waliotawala mchezo huo kwa asilimia 61, huku wenyeji Leicester wakimiliki kwa asilimia 39 .
Wachezaji wa Man City Aleksandar Kolarov ,Kevin De Bruyne, Eliaquim Mangala walipewa kadi njano huku Marc Albrighton wa Leicester nae akipewa kati ya njano na mwamuzi Craig Pawson.
Ligi hiyo itaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa Paka Weusi wa Sunderland watawalika Majogoo wa Jiji la Anfield katika dimba la Light.

No comments:

Post a Comment