tuwasiliane

Tuesday, December 29, 2015

AZAM YAKANA KUTAKA KUMSAJILI NIYONZIMA

Breaking News: Yanga yavunja mkataba na Niyonzima
Klabu ya Azam FC kupitia kwa katibu mkuu wake Idrisa Nassoro umeweka msimamo wake baada ya habari kuanza kuvuma huenda Haruna Niyonzima akijunga na kikosi cha wanalambalamba baada ya Yanga kuvunja mkataba na mchezaji huyo kutokana na utovu wa nidhamu.
Nassoro amesema klabu yao haina mpango wowote wa kumsajili Niyonzima kwasababu tayari inawachezaji saba wa kigeni ambao wanaruhusiwa kikanuni lakini pia tayari hakuna mwanya wa kufanya hivyo kwasababu tayari dirisha la usajili limeshafungwa.
“Sisi hatuhusiki kwa chochote na Haruna wala hatuna mpango wowote na Haruna. Kwanza sheria haituruhusu kwasababu sheria inataka timu iwe na wachezaji saba wa kigeni ambao sisi tayari wote tunao kwahiyo hata tukisema labda Haruna atageukia mlango wa pili aingie Azam, nafasi hiyo hakuna. Kwahiyo hatua mpango wowote na Haruna Niyonzima”,amesema Nassoro.
“Siku za nyuma sisi tulikuwa watu wa mwanzo kabisa, hata mimi nilidiriki kuzungumza na Haruna kabla hata hajaja Yanga, Haruna alikuja hapa na klabu yake ya Rwanda kucheza mashindano ya Kagame nilikaanae lakini mwisho wa siku mwalimu wetu wa kipindi kile hakumuhitaji tukaachananae akaendazake Yanga”.
“Lakini baada ya hapo hakukuwa na mazungumzo tena na Haruna wala mpango wowote wa kutaka kumleta kwenye klabu yetu”.Baada ya Yanga kutangaza kuachana na Haruna Niyonzima kumekuwepo na taarifa za vilabu vya Simba na Azam kutaka kuinasa saini ya kiungo huyo wa Rwanda.

No comments:

Post a Comment