tuwasiliane

Wednesday, December 9, 2015

Majwega amepania kumuumbua Stewart Hall

Majwega Simba
Brian Majwega, amesema atahakikisha anamuonyesha kocha wa Azam FC, Stewart Hall, kipaji alichokuwa nacho.
Anataka kuipa mafanikio Simba na kubeba ubingwa wa Tanzania msimu huu.
Majwega amekiambia chanzo chetu cha habari, anajisikia furaha tangu aidhinishwe kuichezea Simba kwenye ligi ya Tanzania bara hivyo atajipanga kuonyesha makali zaidi ya yale aliyokuwa akiyafanya akiwa na kikosi cha Azam FC.
“Nafuraha kuidhinishwa kuichezea Simba ni timu ambayo nilipenda kuitumikia muda mrefu na pia nataka kumuonyesha kocha wa Azam Hall, kwamba uwezo wangu bado upo juu na siyo kweli kama kimeshuka,”amesema winga huyo raia wa Uganda.
Majwega amekuwa kwenye malumbano na klabu ya Azam tangu kuanza kwa msimu huu kitu ambacho kilimfanya ashindwe kucheza mechi tiza za mzunguko wa kwanza baada ya kocha Hall, kudai hana uwezo na haendani na mfumo anaoutumia na kupelekwa KCCA ya kwao Uganda kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment