tuwasiliane

Wednesday, December 9, 2015

Mkuu wa Google ataka "kichungio cha chuki”

Eric Schmidt

Mkuu wa Google Eric Schmidt amesema kampuni za teknolojia zinafaa kutengeneza programu zenye uwezo wa kuchunga maneno yenye chuki mtandaoni.
Akiandika kwenye New York Times, Bw Schmidt amesema kutumia teknolojia kuzima maneno yenye uchochezi na uenezaji chuki kutasaidia “kupunguza uchochezi katika mitandao ya kijamii” na “kufuta video kabla ya kuenea mtandaoni”.
Maoni yake ameyatoa huku mmoja wa wanaotaka kuwania urais kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton kutoa wito kwa kampuni za Silicon Valley kusaidia kukabiliana na ugaidi, hasa kwa kuunda njia za kukabiliana na kundi linalojiita Islamic State.
"Tunafaa kuwapa kazi watu wanaotengeneza teknolojia za kuvuruga teknolojia nyingine watengeneze njia za kuvuruga ISIS," alisema kwenye hotuba Washington DC.
source.www.bbcswahili.com

No comments:

Post a Comment