tuwasiliane

Wednesday, December 9, 2015

Donald Ngoma ajibashiria kuwa mfungaji Bora Ligi Kuu

Ngoma akishangilia bao lake la kwanza
Straika wa Yanga Donald Ngoma amesema yupo tayari kuendeleza kasi yake ya kufunga mabao kwenye Ligi ya Vodacom, baada ya kufanya mazoezi ya kutosha kwenye kipindi cha mapumziko.
Ngoma raia wa Zimbabwe ameiambia Goal, anataka kuiona timu hiyo ikibeba ubingwa wa msimu huu na yeye kuwa mfingaji bora hivyo amejiandaa katika kila hali kuhakikisha anayatimiza hayo.
“Nimekuja Yanga nikiwa na ndoto ya kuipa mafanikio klabu hii lakini pia kuwa mfungaji bora kama nilivyokuwa FC Platinum, najua linawezekana kutokana na uimara wa timu yetu na mwenendo ambao tumeanza nao katika ligi ya msimu huu,”amesema Ngoma.
Ngoma amesema kwa namna ambavyo amejiandaa anauhakika mkubwa wa kufunga katika mechi mbili watakazo cheza Tanga kuanzia wikiendi hii wakianzia na ile ya Jumamosi Desemba 12 dhidi ya Mgambo JKT na African Sports itakayopigwa Jumatano ijayo uwanja wa Mkwakwani.
source.www.goal.com

No comments:

Post a Comment