tuwasiliane

Thursday, December 10, 2015

KIFAA KIPYA CHA YANGA NA REKODI ZAKE ZA KUTISHA

PicsArt_12-09-10.19.04
Wakati pilikapilika za usajili wa dirisha dogo zikiwa zimepamba moto, mabingwa watetezi wa taji la ligi ya Vodacom Tanzania bara Yanga SC jana usiku imempokea kiungo wa kimataifa wa Niger Issoufou Boubacar Garba tayari kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo ambaye atachukua nafasi ya mbrazil Andrey Coutinho aliyefunguliwa mlango wa kutokea Jangwani.
Garba amewasili jana na leo alipelekwa kwenye mazoezi ya Yanga tayari kuanza majaribio ili kama benchi la ufundi la timu hiyo litaridhishwa na kiwango chake basi atapewa kandarasi ya kukitumikia kikosi hicho cha mitaa ya TwigaYanga inakabiliwa na michuano ya kimataifa ikiwa inatarajiwa kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika mashindano makubwa kwa upande wa Afrika kwa ngazi ya vilabu.
Na huu ndiyo wasifu wa mchezaji huyo;
Garba amepita kwenye timu kadhaa lakini timu yake ya kwanza kuitumikia ilikuwa ni AS FAN ambako alijiunganayo mwaka 2010 lakini hakupata nasafi ya kucheza hata mchezo mmoja kwenye timu hiyo hadi alipojiunga na klabu ya Muangthong United ya nchini Thailand ambako pia hakupata nafasi ya kucheza mchezo hata mchezo mmoja.
Mambo hayakuishia hapo, mchezaji huyo akaendelea na safari yake ya kutafuta mafanikio katika soka ambapo mwaka huohuo alijiunga na klabu ya Phuket ambako alikaa hadi mwaka 2012 bila kucheza hata mchezo mmoja kwenye timu hiyo.
Mwaka 2012 alijiunga na klabu ya Club Africain lakini bado jinamizi la kutopata nafasi ya kucheza kwenye vilabu alivyojiunga navyo lilizidi kumwandama kwani hata kwenye timu hii bado hakupata nafasi ya kucheza hata mchezo mmoja. Mwaka huohuo akasajiliwa na klabu ya ES Hammam-Sousse lakini bado hali iliendelea kuwa tete kwa mchezaji huyo kutokana na kuendelea kusugua benchi. na Jangwani.
Mchezaji huyo amezaliwa February 2, 1990 kwenye mji wa Niamey, Niger amewahi kupita kwenye vilabu kadhaa lakini hata hivyo hakupata nafasi ya kucheza kwenye vilabu hivyoMchezaji huyo ameitumikia timu yake ya taifa ya Niger katika mechi 17 katika kipindi cha mwaka 2011 na kufanikiwa kufunga magoli mawili (2) lakini bado haijafahamika kama bado anaendelea kuitumikia timu yake ya taifa hadi leo.
Katika kipindi cha usajili wa dirisha kubwa klabu ya Yanga ilimsajili mchezaji Joseph Tetteh Zuttah lakini mchezaji huyo alishindwa kuonesha makali kwenye kikosi hicho mwisho wa siku akapigwa chini. Siku chahe zilizopita uongozi wa Yanga ulivunja mkataba na Andrey Coutinho kwa madai kwamba kiwango chake kimeshindwa kumvutia mwalimu wa timu hiyo Hans van Pluijm.
CV ya mchezaji huyu inaonesha hajapata nafasi ya kucheza kwenye kila timu aliyopita, swali ni je, ataweza kuonesha makali akiwa ndani ya uzi wa njano na kijani? Majibu yote yataonekana uwanjani, mpira unachezwa uwanjani kila mtu ataona uwezo wa mchezaji huyo.
Huu ndiyo wasifu wa Issoufou Boubacar Garba kwa ufupi unaoonesha safari yake ya soka na timu ambazo amewahi kupita mchezaji huyo.

Issoufou Boubacar
Personal information
Full nameIssoufou Boubacar Garba
Date of birth2 February 1990 (age 25)
Place of birthNiameyNiger
Height1.68 m (5 ft 6 in)[1]
Playing positionMidfielder
Club information
Current teamES Hammam-Sousse
NumberTBA
Senior career*
YearsTeamApps(Gls)
2010AS FAN(-)
2011Muangthong United(-)
2011–2012Phuket(-)
2012Club Africain0(0)
2012–ES Hammam-Sousse0(0)
National team
2011–Niger17(2)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only.
source shaffihdauda

No comments:

Post a Comment