tuwasiliane

Thursday, December 10, 2015

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA


Rais muh John Pombe Magufuli ametangaza baraza
 jipya la mawaziri,Kwa mujibu wa muheshimiwa magufuli amesema
 Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.katika uteuzi huo Dr Magufuli ameteua kama ifuatavyo;
WIZARA
Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo

Mazingira: Makamba, naibu Makamba

Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma

Ulemavu: Mavunde

Kilimo, mifugo na uvuvi: Mwigulu Lameck Nchemba, Nashe naibu

Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani.

Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi

Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu

Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe

Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nmemteua mbunge na waziri,

Ulinzi na kujenga taifa: Waaziri Dr. Hussein Mwinyi

Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

Utalii: Waziri bado

Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage

Sayansi na ufundi: Naibu ni Stella Manyanya

Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala

Habari: Nape Nnauye

Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa, Naibu ni Kamwene

No comments:

Post a Comment