tuwasiliane

Friday, December 11, 2015

Jamuri Kihwelo atamba Mwadui FC haiwezi kumfukuza

Jamhuri Kihwelo 'Julio'
KOCHA wa Mwadui FC Jamuri Kihwelo ‘Julio’ amesema hawezi kufukuzwa kwenye timu hiyo kutokana na mwenendo mzuri wa timu hiyo kwenye Ligi ya Vodacom Tanzania.
Julio amekiambia chanzo chetu cha habari kuwa,, timu yake imekuwa ikitoa upinzani mkubwa kwa timu kubwa za Yanga, Azam na Simba hivyo bado anamuda mrefu wa kuwa kuifundisha timu hiyo inayomilikiwa Kampuni ya uchimbaji madini iliyopo Shinyanga.
“Najua kile kwenye mafanikio hapakosi fitina napata changamoto kubwa kuwepo kuwa kocha wa Mwadui, lakini hilo halinitishi ninachoweza kusema Mwadui itaendelea kufanya vizuri chini yangu wapinzani wasubiri mwishoni mwa msimu kuona tutamaliza kwenye nafasi gani,” amesema Julio.
Mwadui ipo nafasi ya saba (7) kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 10, timu hiyo imeweza kushinda mechi nne na kutoka sare michezo mitatu na kupoteza michezo mitatu hadi.

No comments:

Post a Comment