tuwasiliane

Friday, December 11, 2015

MWANASOKA BORA WA BBC HADHARANI LEO

Tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka inayoandaliwa na BBC, itawekwa hadharani hii leo. Mwandishi wa BBC Peter Okwoche ndiye aliyeteuliwa kukabidhi tuzo hiyo na ndiye mwenye bahasha yenye maelezo ya mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu.
Watatu kati ya watano waliopenya katika mchujo walioteuliwa kuwania tuzo hiyo wanabashiriwa kushinda kwa mara ya pili na hivyo inajumuisha mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka uliopita, Mu Algeria Yacine Brahimi ambaye amefanya vizuri mwaka huu akiwa na klabu yake ya FC Porto.
Mwingine anayebashiriwa kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili ni mchezaji wa timu ya Swansea Andre Ayew, ambaye aliiwezesha timu ya Ghana kufanikiwa kutinga katika fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. Mwingine ni Yaya Toure wa timu ya Manchester City na Ivory Coast, ambaye alitwaa tuzo ya mchezaji bora barani mwezi Februari mwaka huu.
Mwingine ambaye naye pia anatajwa kutwaa tuzo hiyo ni mshambuliaji wa timu za Gabon na Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye amekuwa akifumania nyavu tangu mwaka huu uanze.
Hata hivyo, msenegali Sadio Mane ambaye ameingia katika orodha ya mwisho kwa mara ya kwanza baada ya kufanya mambo makubwa akiwa na timu ya Southampton mwaka huu, mwaka mmoja alipofunga bao tatu katika ligi yenye ubavu wa haja na kasi uwapo uwanjani na kuandika historia.
Nayo Tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika inapigiwa kura na mashabiki wa soka ulimwenguni, ambapo mwezi uliopita upigaji kura ulifungwa rasmi mwezi uliopita.
Mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu atatangazwa tarehe 24 katika historia na itaoneshwa katika runinga ya BBC World TV, World Service radio na katika mitandao ya BBC saa kumi na mbili na dakika arobaini na Tano kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment