tuwasiliane

Friday, December 11, 2015

BOCCO;Simba bado haijawa na kiwango cha kupambana na sisi”-

“Simba bado haijawa na kiwango cha kupambana na sisi”- John Bocco
Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 25, na Simba inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 21
Kikosi cha vinara wa Ligi ya Vodacom Azam FC, kimeendelea kujifua kwa nguvu kujiandaa na pambano la Jumamosi dhidi ya Simba, huku wakiwa wamedhamiria kupata ushindi.
Nahodha wa timu hiyo John Bocco, amekiambia chanzo chetu cha habari kuwa wanataka kudhihirisha ubora wao kupitia mchezo huo ambao lengo lao kubwa ni kupata ushindi utakao waweka kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kuongoza ligi.
“Tunafanya mazoezi ya nguvu lengo ni kushinda na kuonyesha dhamira yetu ya ubingwa msimu huu, Simba ni timu nzuri lakini bado haijawa na kiwango cha kupambana na sisi kutokana na uimara wa kikosi tulichonacho msimu huu,” amesema Bocco.
Bocco amesema kikosi chao chote kimekamilika kwa sasa hivyo bado hajaona ni namna gani wapinzani wao Simba wanaweza kuepuka na kipigo kutokana na dhamira waliyokuwa nayo ambayo ni kuchukua ubingwa na kuzifunga timu kubwa.
Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 25, na Simba inashika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 21 hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali.

No comments:

Post a Comment