tuwasiliane

Thursday, December 31, 2015

Dylan Kerr amesema yupo tayari kuachana na Simba

Kocha Dylan Kerr, amesema yupo tayari kuachana na klabu ya Simba kwa sababu ya viongozi na mashabiki wa timu hiyo kutothamini kile anachokifanya hivi sasa.
Kerr ameiambia Goal, anajua kama kama kuna mpango wa chinichini unafanywa na viongozi kuletwa kocha mpya atakaye  nafasi yake ya kuifundisha timu hiyo aliyoitoa mbali baada ya kumaliza nafasi ya nne msimu uliokwisha.
“Sina hofu ukocha ndiyo kazi yangu nipo tayari kuiacha Simba na kutoa nafasi kwa kocha mpya atakayeletwa na uongozi kwasababu najiamini na taaluma yangu na siwezi kukosa kazi ya kufanya iwe ndani au nje ya Tanzania,”amesema Kerr.
Pamoja na kutoaminiwa lakini timu hiyo bado haijafanya vibaya licha ya kuwa nafasi ya nne kwenye msimamo kwa idadi ya pointi ilizokuwa nazo na zile walizokuwa nazo timu mbili za juu ni tofauti ya mechi mbili kitu ambacho siyo tatizo kwasababu ligi bado inaendelea.
Kocha wa zamani aliyeifundisha timu hiyo msimu uliopita Mserbia Goran Kopunovic ndiye anayepewa nafasi ya kuifundisha timu hiyo kigezo kikubwa kikiwa ni kuibadili timu hiyo kwa kipindi kifupi alichoifundisha akichukua nafasi ya Mcroatia Zrogan Logaruzic.Dylan Kerr, amesema yupo tayari kuachana na klabu ya Simba anayoifundisha hivisasa kwasababu ya viongozi na mashabiki wa timu hiyo kutothamini kile anachokifanya hivi sasa.
Kerr ameiambia Goal, anajua kama kama kunampango wa chinichini unafanywa na viongozi kuletwa kocha mpya atakaye chukua nafasi yake ya kuifundisha timu hiyo aliyoitoa mbali baada ya kumaliza nafasi ya nne msimu uliokwisha.
“Sina hofu ukocha ndiyo kazi yangu nipo tayari kuiacha Simba na kutoa nafasi kwa kocha mpya atakayeletwa na uongozi kwasababu najiamini na taaluma yangu na siwezi kukosa kazi ya kufanya iwe ndani au nje ya Tanzania,”amesema Kerr.
Pamoja na kutoaminiwa lakini timu hiyo bado haijafanya vibaya licha ya kuwa nafasi ya nne kwenye msimamo kwa idadi ya pointi ilizokuwa nazo na zile walizokuwa nazo timu mbili za juu ni tofauti ya mechi mbili kitu ambacho siyo tatizo kwasababu ligi bado inaendelea.
Kocha wa zamani aliyeifundisha timu hiyo msimu uliopita Mserbia Goran Kopunovic ndiye anayepewa nafasi ya kuifundisha timu hiyo kigezo kikubwa kikiwa ni kuibadili timu hiyo kwa kipindi kifupi alichoifundisha akichukua nafasi ya Mcroatia Zrogan Logaruzic.

No comments:

Post a Comment