tuwasiliane

Monday, June 23, 2014

RAIS WA BUGANDO APATIKANA USIKU akutwa akiwa katupwa Usagala Akiwa hajitambui na akiwa amepoteza kumbukumbu

                      pichani ni Mdede kabla hajatekwa
 
 
 
Rais wa chuo kikuu Bugando Mussa Leonard Mdede amepatikana usiku akiwa hajitambui na amepelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwaajili ya vipimo na matibabu zaidi,bwana Mdede ambaye pia ni mwenyekiti wa TAHILISO nchini alitoweka tangia tarehe 18 mwezi huu saa kumi jioni,na haikuweza kufahamika mara moja yupo wapi na kama ametekwa nani kamteka, mpaka usiku huu taarifa za kupatikana kwake zilipotufikia.

Akiongea na mwandishi wa habari hii,waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Bugando Benjamini Thomas,alisema Mdede aliletwa na vijana watatu,wanaume wawili na mwanamke mmoja waliodai kumuokota bwana Mdede katika eneo la Usagala akiwa hajitambui wala kujielewa,anaendelea kusema kwa mujibu wa mama mwenye Nyumba wa Mdede,watu hao walidai baada ya kumuokota jana usiku katika eneo hilo la Usagala,waliamua kumchukua na kwenyda kumuhifadhi katika eneo la Igoma, alipoanza kupata fahamu na kueleza anaishi wapi ndipo wakamleta nyumbani kwake,huku watu hao wakidai walishindwa kumleta jana na asubuhio kutokana na Mdede kutojitambua na kuwa katika hali ya kupoteza kumbukumbu,hata hivyo mama  mwenye nyumba  anasema watu hao hawakukaa sana wakaondoka bila kutoa maelezo zaidi.

Waziri mkuu huyo wa Bugando aliendelea kusema,"kwa mujibu wa mama mwenye nyumba,alisema kwamba mara baada ya watu hao kumleta nyumbani hapo wakiwa wamempakia kwenye gari aina ya Kenta,walitoa maelezo machache na hawakutaka kukaa sana wakaaga wakaondoka ",mwandishi wa habari hii alipotaka kujua kwamba ni  mtu gani alikuwa wa pili kupata taarifa hizo kabla  ya yeye waziri mkuu,alisema ni kaka zake Mdede na ndugu zake wengine,alisema mmoja wa kaka yake Mdede anayefanya kazi katika moja ya bank iliyopo jijini hapa,alipata taarifa za kupatikana kwa mdogo wake akiwa kazini,lakini alinyimwa ruhusa ya kuondoka kazini mpaka pale alipolazimisha kuondoka,anaendelea kusema kaka yake Mdede alipofika kwenye Nyumba aliyopanga Mdede alimkuta mdogo yake akiwa hajielewi wala kujitambua japo hakuwa na jeraha lolote mwilini.

Kwa mujibu wa waziri mkuu Thomas anasema kaka yake alijaribu kuwapigia mara kadhaa lakini yeye hakupokea simu yake kwakuwa alikuwa anatoa tamko kwa waandishi wa habari juu ya kupotea kwa Mdede,na walipomaliza kutoa tamko walielekea kwa Mdede baada ya kuambiwa na kaka yake kila kitu,"na tulimkuta anamwonekano, anahali dhoofu,akiwa anaongea kwa tabu na huku akiwa hana kumbukumbu nzuri zaidi ya kumbukumbu ya kabla hajatekwa"anaendelea kusema waliwasiliana na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Nyamagana na wakakubaliana wasitoe taarifa kwanza mpaka watakapo muhoji na kuangalia taratibu zingine za kiulinzi,na baadae ndipo walipojiridhisha na kuamua kumpeleka hospitalini Bugando kwani awali alikuwa akipatiwa matibabu palepale nyumbani kwake,lakini waliamua kumpeleka hospitali hiyo kwa ajili ya vipimo na uchunguzi zaidi na hasa walipoona hali ya Mdede haieleweki na wakahisi huenda akawa amelishwa vitu vibaya kama sumu.

Mpaka sasa bwana Mdede hana kumbukumbu na hajui kipi kilichomtokea na wala hajui alikuw awapi.
SOURCE; http://www.paparazihuru.com/

No comments:

Post a Comment