tuwasiliane

Thursday, June 12, 2014

POLISI AUWAWA BAADA YA MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO CHA POLISI

 


Majambazi wanaokisiwa kuwa sita, wakiwa na pikipiki tatu, juzi walivamia Kituo Kidogo cha Polisi Mkamba kilichopo Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga, Pwani na kuua askari mmoja na mgambo na kujeruhi mgambo mwingine na kisha kupora bunduki tano na risasi 60 usiku wa kuamkia juzi.
Polisi aliyeuawa ni Konstebo Joseph Ngonyani na majeruhi Venance Francis na Mariamu Mkamba ambao walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya Mkuranga kwa matibabu.
Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, majambazi hayo yalikuwa na taarifa kwamba kituo hicho kina silaha za moto na kuweka mpango wa kukivamia usiku baada ya kupiga hesabu na kujiridhisha kwamba polisi kutoka Kibiti, wilayani Rufiji au Mkuranga wasingeweza kufika hapo kabla ya wao kutekeleza azma yao.
Mkazi wa Kimanzichana, Mohamedi Muba alisema wananchi wenzake walimwambia kuwa majambazi hayo yalifika kituoni hapo saa saba usiku na kuvamia kituo hicho wakitaka funguo za kufungulia stoo zilipohifadhiwa silaha.
“Kituo cha Kimanzichana kipo mbali sana na vituo vingine vya Kibiti na Mkuranga, ni kama kilometa 30 hadi 35, hivyo kwa wakati huo wa usiku wa manane ingekuwa vigumu kuwahi kutoa msaada,” alisema mkazi mwingine ambaye hakutaka kutajwa jina.
Mkazi huyo alisema baada ya kubishana na askari huyo aliyekuwa na ufunguo, majambazi hayo yalitumia nguvu kumlazimisha kutoa funguo.
Huku mzozo huo ukiendelea, majambazi wengine walikuwa wakiwashambulia askari mgambo kwa mapanga na walipoona askari amegoma kutoa funguo walimpiga risasi na kuzichukua kisha kufungua na kuchukua silaha na kutokomea kusikojulikana.
Alisema majambazi hayo yalionekana kujipanga na kuwa na taarifa zote kuhusu hali ya ulinzi katika kituo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema ameagizwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Paul Chagonja kwamba ndiye atakayelizungumzia suala hilo.
“Kwa sasa nipo chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ninashughulikia mwili wa askari aliyeuawa, Makao Makuu watalizungumzia zaidi,” alisema Kamanda Matei.
Chagonja alonga
Akizungumzia tukio hilo jana, Chagonja alisema majambazi hayo waliojifanya kuwa ni raia
wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kiman

nanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha
za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa
ni watu wanaohitaji msaada. Cha kushangaza
watu hao walimvamia askari mwenye silaha
ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH
NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga
na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi
30. Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi
askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya
pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora
risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.
Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa
anapatiwa matibabu kwenye hospitali wilaya ya
Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE
amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado
imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni

na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana
mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa
mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo
aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha

No comments:

Post a Comment