tuwasiliane

Thursday, June 12, 2014

MGOMO WA WAFANYAKAZI WA UWANJA WA NDEGE WA RIO,BRAZIL


Wafanyakazi wa kiwanja cha ndege cha Rio wametangaza mgomo wa saa 24 kuanzia usiku wa manane saa za Brazil.
Hii ni kumaanisha mgomo huo utaendelea hadi wakati wa ufunguzi wa kombe la dunia.
Japo sherehe na mechi ya ufunguzi zinafanyika mjini Sao Paulo, na ni asilimia 20% tu ya wafanyikazi ndio watakao goma, mgomo huo bila shaka utatatiza usafiri katika mji huo wa Rio ulio wapili kwa ukubwa nchini Brazil.

Wafanyikazi wanaoshughulikia abiria na mizigo na wale wanaofanya usafi wa hata ndegeni ni baadhi ya watakaogoma.
 
 
Afueni baada ya baadhi ya wabrazil wafanyikazi wa reli na mabasi kusitisha migomo ya kudai posho.

Sehemu za kuhudumia wageni wa kimataifa na wa ndani ya nchi zitatatizwa na mgomo huo.
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara na posho za kufanya kazi wakati wa kombe la dunia wakisema kazi zimeongezeka.
Mmoja wa viongozi wa chama cha wafanyikazi hao , Luiz Braga, amekana wanatatiza kombe la dunia kwa maksudi, akieleza kuwa 'hatutaki kuharibu kombe la dunia, tunachofanya ni kudai haki zetu tu'.

No comments:

Post a Comment