tuwasiliane

Monday, June 30, 2014

PIGO KWA UJERUMAN;PODOLKI MAJERUHI SASA KUKOSA GAME YA UJERUMANI NA ALGERIA


Mshambulizi wa Ujerumani na Arsenal ya Uingereza Lukas Podolski hatoweza kushiriki mechi ya mkondo wa pili kati ya Ujerumani na Algeria iliyoratibiwa kuwa Porto Alegre.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye anashiriki kombe lake la tatu la dunia inasemekana kuwa alijeruhiwa katika mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Marekani .

Sasa madaktari wa timu hiyo inayopigiwa upatu kufuzu kwa fainali ya kombe la dunia mwaka huu wanasema kuwa anahitaji angalau siku mbili au tatu kupumzika ilipaja lipate nafuu na hiyo inamaanisha kuwa kocha Joachim Loew
sasa atalazimika kumchezesha mshambulizi mwengine upande wa kushoto .Kutokuwepo kwa Podolski sasa kutampatia mshambulizi wa Bayern Munich ya Ujerumani Mario Goetze nafasi ya kutawala dhidi ya Algeria.
Kikosi cha Loew kingali kinasuri habari kumhusu kiungo wa upande wa kulia Jerome Boateng ambaye pia hakuweza kushiriki mazoezi yao ya mwisho kutokana na jeraha la goti.
Ujerumani itachuana na the Desesrt Foxes ya Algeria jumatatu katika uwanja wa Porto Alegre’s Beira-Rio .

No comments:

Post a Comment