Wachezaji saba wa Costa Rica waliolazimishwa na
maafisa wa FIFA kupimwa mkojo punde baada ya ushindi wa kihistoria dhidi
ya Italia wamedhibitishwa kuwa hakutumia dawa za kuongeza nguvu
mwilini.
Maafisa wa Afya na wale wa kuchunguzi utumiaji
wa madawa ya kututumua misuli yaliyopigwa marufuku walliwavamia
wachezaji punde baada ya ushindi huo mkubwa na kuwatenga hadi pale
walipochukua mkojo kwa ajili ya kupima chembe chembe za damu .Awali wachezaji kadha walilazimika kupimwa punde baada ya mechi ambayo Costa Rica iliizaba Uruguay mabao 3-1.
Mfumo huu wa kupima mkojo wa wachezaji punde baada ya mechi imeiwacha FIFA ikishtumiwa kwa kupendelea timu fulani kushamiri katika kombe la dunia huku timu ambazo hazikutarajiwa kunawiri zikishurutishwa kupimwa dawa za kututumua misuli zilizopigwa marufuku.
Aliyekuwa mchezaji wa wa Argentina Diego Maradona aliiunga shirikisho la soka la Costa Rica kuikashifu FIFA akisema mbinu hiyo mpya inalenga kuwazonga wachezaji na mawazo kabla ya kipute hicho kumalizika nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment