tuwasiliane

Monday, June 9, 2014

Filippo Inzaghi kocha AC MIlan


 

 


AC Milan imemfuta kazi mkufunzi wake Clarence Seedof baada ya kuhudumu kwa chini ya miezi 5 na kumtangaza Filipo Inzaghi kama kocha mpya.

Seedof mwenye umri wa miaka 38 alikuwa amechukua nafasi yake Massimiliano Allegri mwezi Januari, wakati timu hiyo ilikuwa katika nafasi ya 11 katika ligi kuu ya Italia Serie A na alama 30 nyuma ya viongozi wa wakati huo Juventus, ambao walishinda taji hilo mwisho wa msimu.
 
Hata hivyo, mholanzi huyo alishindwa kubadili mkondo na msururu wa matokeo duni uliendelea hadi mwisho wa msimu timu hiyo ilipomaliza ikiwa na alama 45 nyuma ya mabingwa msimu huu Juventus.

No comments:

Post a Comment