tuwasiliane

Monday, June 9, 2014

MGOMO WA WAFANYAKAZI WA USAFIRI WAZIDI KUENDELEA BRAZIL

Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa mda usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama ya leba nchini humo, iliyokuwa imewaamuru wafanyikazi hao kurudi kazini mara moja.

Koti ilikuwa imesema wakuu katika vyama vya wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walikuwa wametumia mamlaka yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita.
Huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari umezidi kuizonga Sao Paulo.
 
Sasa wasiwasi unaongezeka, wa Je hali ikiendelea hivyo itakuaje hapo alhamisi wakati jiji hilo ndilo linafungua dimba hilo?
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.

No comments:

Post a Comment