tuwasiliane

Tuesday, June 24, 2014

BRAZIL KUIKABILI CHILE,KTK RAUNDI YA PILI,MTOANO

Neymar alifunga mara mbili katika mechi aliyokuwa mchezaji bora wakati Brazil ilipoishinda nguvu Cameroon na kufuzu katika raundi ya muondoano.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga mabao 2 katika kipindi cha kwanza baada ya bao la kusawazisha lake Joel Matip, huku Fred na Fernandinho wakihakikishia timu hiyo nafasi katika mkondo wa pili wa timu 16 bora kama washindi wa kundi A.
Kushiriki kwa Brazil katika robo fainali kunategemea mechi yao dhidi ya Chile katika robo fainali, na Brazil watakwenda katika mechi hiyo itakayochezewa jijini Belo Horizonte siku ya Jumamosi wakiwa na imani mpya ya kunyakua taji hilo.

Matokeo duni dhidi ya Croatia na Mexico yameibua wasiwasi kuhusu Brazil - na hofu inasalia katika safu yao ya ulinzi - lakini Neymar akiwepo, chochote chaweza kutokea.
Mshambulizi huyo wa Barcelona alirejea na bao dhidi ya Japan katika mechi ya ufunguzi katika mechi ya kwanza ya Kombe la Mashirika la mwaka uliopita, ambayo iliisaidia Brazil kuanza kwa ushindi ili kunyakua taji hilo, na kocha Luiz Felipe Scolari atatumai kuwa matokeo haya yatakuwa na athari sawa.


Brazil ilikuwa karibu kupata bao la kwanza mkwaju wake Paulinho ulipozuiliwa baada ya Hulk kumpigia pasi iliyokuwa imetoka kwake Neymar, lakini tamaa yao ya kushambulia ikawafanya kusahau safu ya ulinzi, ambayo Cameroon ilonekana kutaka kutumia.
Marcelo aliokoa mkwaju ambao angefunga Vincent Aboubakar kabla ya David Luiz kulazimika kuondoa mkwaju aliokuwa ameupiga Eric Choupo Moting katika eneo la lango.
Hata hivyo, Brazil walionekana wasiokata tamaa, Luiz Gustavo alipata mpira katika ubavu wa kushoto na kumpigia pasi Neymar ambaye alimpiku Charles Itandje na kufunga bao.
Ilikuwa njia nzuri ya kuandikisha bao la 100 katika Kombe la Dunia - na mchezaji yuyo huyo alikaribia kufunga bao la pili ambalo Itandje aliondoa.
Uwanja uliokuwa umejaa kelele ulinyamaza kimya wakati Cameroon walipoweka wazi safu hafifu ya ulinzi ya Brazil, Nyom akimpiku Dani Alves na kumpigia pasi Matip aliyefunga kwa karibu.
Scolari aliwaashiria wachezaji wake, nao wakamjibu kwa njia ya pekee wanayojua, Marcelo kumpigia Neymar pasi ambaye alikimbia na kuwapiga chenga mabeki 2 wa Cameroon na kufunga bao lake la 35 katika mechi 52 za kimataifa.


Scolari alimwondoa Paulinho na kumweka Fernandinho wakati wa mapumziko .
Kiungo huyo wa Manchester City alichangia nipe nikupe iliyozaa bao lake Fred .
Fernandinho alifunga bao la nne na kuonyesha kuwa kuwepo kwake kulichangia ushindi huo.

No comments:

Post a Comment