Samatta
kulia na Ulimwengu kushoto wakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Kikwete hivi karibuni mjini Kinshasa, DRC. Wachezaji
hao wamewasili mchana wa leo kujiunga na StarsWashambuliaji
hao wa Taifa Stars wamewasili saa 7.25 mchana kwa ndege ya Ethiopian
Airlines wakitokea Khartoum, Sudan ambapo jana (Mei 16 mwaka huu) timu
yao ya TP Mazembe ilicheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al
Hilal ya huko na kufungwa 1-0.
Katika
mchezo huo wa kwanza wa Kundi A na wa kwanza kwa ujumla hatua ya
makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, washambuliaji wote hao wawili wa
Tanzania walicheza, Samatta akianza na
Ulimwengu akitokea benchi dakika ya 66 kwenda kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.
Kocha
wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili
ya mechi hiyo, kwani kimepata mechi za kirafiki na mazoezi ya kutosha
kwenye kambi iliyoanzia Tukuyu mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu
mkubwa.
Naye
Kocha Msaidizi wa Zimbabwe, Kalisto Pasuwa amesema hawaifahamu vizuri
Taifa Stars lakini wamekuja kwenye mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni
kwa ajili ya kushinda, na kuwataka washabiki wajitokeze kwa wingi kuona
kiwango cha timu yake.
Milango
kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana
wakiongozwa na Joseph Odartei Lamptey itakuwa wazi kuanzia saa 6 kamili
mchana, na tiketi zitapatikana katika magari maalumu uwanjani hapo.
Viingilio
katika mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na
bluu, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 20,000 kwa VIP A.
| | | |
No comments:
Post a Comment