tuwasiliane

Saturday, May 17, 2014

ARSENAL KUSAFISHA NYOTA LEO?

Timu ya Arsenal ina matumaini ya kumaliza kiu chake cha miaka tisa bila taji lolote baadaye hii leo wakati itakapochuana na timu ya Hull City katika mechi ya fainali ya kombe la F.A katika uwanja wa Wembley nchini Uingereza.

Gunners ilishinda taji lake la mwisho mwaka 2005 katika fainali za kombe la F.A ambapo iliwacharaza wapinzani wao wa jadi Manchester United katika mechi iliochezewa katika uwanja wa Cardiff,huku timu ya Hull City ikishiriki kwa mara ya kwanza katika fainali ya kombe hilo.

Meneja Arsene Wenger ameshinda mataji saba muhimu katika miaka yake 18 kama mkufunzi wa timu ya Arsenal, ikiwemo mataji matatu ya ligi kuu ya uingereza pamoja na manne ya kombe la F.A.
Mechi hiyo itaanza mwendo wa saa moja saa za afrika mashariki mbele ya mashabiki elfu tisaini watakaojaa katika uwanja wa Wembley.

Mashabiki wa timu zote mbili walikabidhiwa tiketi 25,000 kila moja huku tiketi nyengine 20,000 zikipewa watu waliojitolea katika mashirika ya hisani,vilabu na ligi za kaunti.

No comments:

Post a Comment