Siku
chache baada ya kuchaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki
duniani, Papa Francis amewashangaza wengi mengi kwa kukataa kuvaa viatu
vya kifahari na msimamo wake kuwekwa wazi kuwa hatavumilia makasisi
watakaotenda uovu.
Tayari, Papa Francis ameelezwa kuwa kiongozi
asiyetaka makuu, mhafidhina na mtu ambaye hataweza kubadili mengi katika
kanisa hilo lenye waumini bilioni 1.2 duniani.
Katika siku mbili za uongozi wake, Papa Francis
amelithibitisha hilo kwa kutokea hadharani akiwa amevaa viatu rahisi,
vyeusi na kuachana na vyekundu vya kifahari vilivyopendelewa na
mtangulizi wake, Benedict VXI.
Katika uongozi wake, siku zote Papa
Benedict, alivaa viatu vyekundu vilivyotengenezwa kwa mkono, jambo
ambalo Papa Francis anaonekana kuachana nalo.
Watu walio karibu naye Papa Francis, wanaeleza
kuwa kabla ya kuondoka Buenos Aires, Argentina kwenda Rome, Kardinali
Jorge Mario Bergoglio, kama alivyojulikana awali, alivaa viatu rahisi
vya rangi nyeusi, na kuwafanya marafiki zake, wakiwamo mapadri kutaka
kumnunulia viatu vingine vipya.
“Siku ile aliyoondoka mjini Buenos Aires kuelekea
Rome kwa ajili ya mkutano wa uchaguzi wa Papa (conclave), marafiki zake
walimpa zawadi ya viatu. Yeye, siku zote amekuwa akitokea hadharani
akiwa amevaa nguo rahisi, viatu vya kawaida,” walieleza mapadri hao
kutoka Amerika Kusini walipozungumza na Kituo cha Redio Vatican.
Mbele ya makardinali 106
Juzi Ijumaa alipokutana na makardinali 106,
kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76, licha ya kuonyesha uso wa furaha
na kuwatania aliwaonya makardinali hao kuhusu wajibu wao kama viongozi
wa kanisa maeneo mbalimbali duniani akiwataka kutosahau kuwa hawarudi
kwenye ujana.
Katika ukumbi wa Sala Clementina, ulioko Vatican
Papa Francis pia aliwataka makardinali hao wakiwamo waliomchagua
kuwategemea zaidi vijana aliosema ndio nguzo kuu muhimu ya ustawi wa
Kanisa Katoliki, huku aliwashauri makardinali kusaka njia sahihi ya
kueneza Ukristo pande zote za uso wa dunia katika karne ya 21.
Aidha, alimsifu mtangulizi wake, Papa Benedict kwa
uamuzi wa kijasiri wa kustaafu, akieleza kuwa ni uamuzi wa busara,
wenye kuonyesha ukomavu na kuwataka wasichoke kuiga matendo mema.
Yaliyomo kitabuni mwake
source;www.mwanchi.co.tz

No comments:
Post a Comment