Mbali na mchakato huo, tayari nchi hizo
zimeshapitisha mfumo wa kisheria utakaowezesha nchi wanachama kuwa na
mfumo wa pamoja wa utambuzi wa sifa za elimu na taaluma mbalimbali ndani
ya jumuiya hiyo.
Akifungua Kongamano la Biashara la Wanafunzi wa
Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Uledi Mussa alisema kuwa hatua hiyo itawapa uhuru
wananchi wa nchi wanachama kufanya kazi na shughuli nyingine za
kibiashara katika nchi yeyote Afrika Mashariki.
“Hatua hii itasaidia wananchi kutoka nchi
wanachama kuvuka mipaka na kwenda kutafuta kazi na shughuli yeyote
katika nchi wanachama bila kupewa visingizio vya kuwa elimu yake
haiendani na mfumo wa elimu wa nchi anayoombea kazi” alibainisha Mussa.
Alisema licha ya kuwa hivi sasa kuna mifumo
tofauti ya elimu na mitalaa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, bado vijana wanatakiwa kupewa taaluma na ujuzi
utakaowawezesha kupambana na changamoto za ukosefu wa ajira.
Alisema kuwa familia na jamii kwa jumla wanatakiwa
kuwapa vijana mahitaji binafsi yaliyojengeka katika misingi ya
kimaadili jambo litakalowasaidia kufa nya kazi na kuishi katika maisha
mazuri.
Naye Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi cha
nchini Kenya, Michael Megoh alisema kwamba mfumo wa elimu wa nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unawapa shida wanafunzi wengi
pale wanapotaka kusoma katika baadhi ya vyuo katika nchi hizo.
Mshiriki wa kongamano hilo
rian Matara alisema mitalaa mingi ndani ya nchi za
EAC haipitiwi mara kwa mara ili kwenda na wakati na kwamba kuna haja ya
kuandaa mfumo wa elimu na mitalaa itakayoongeza ujuzi.
No comments:
Post a Comment