Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21
kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya
mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim
amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu
ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.
“Itakuwa
mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili
yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco.
Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka
kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza
fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya
mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea
nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory
Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la
Dunia.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco,
Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi
ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu
nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
Wachezaji
aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini
Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam),
Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga),
Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa
Sugar).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga),
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam),
Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho
Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
No comments:
Post a Comment