Na Baraka Mbolembole, Aliyekuwa Morogoro
Kwa
takribani miaka sita nimekuwa karibu na kambi ya Simba Sports Club,
hasa inapokuwa inakabiliwa na michezo katika Manispaa ya Morogoro. Kabla
sijaanza kuandika nilipenda kuwa karibu na timu hiyo kwa sababu ya
kujifunza baadhi ya maisha ya wachezaji wa ligi kuu. Zaidi mimi ni
mshabiki wa timu hii tangu kuzaliwa kwangu. Nikaona ni bahati kubwa kwa
timu ya ndoto kuja mtaani kwetu na kuweka kambi ya muda mrefu wakati ule
uwanja wa Uhuru, ulipofungwa kwa matengenezo madogo.
Na
hata wakati ule wa michuano ya ligi kuu ndogo, kwani, Simba, ilikuwa
imepangwa katika kituo cha Morogoro. Mida ya asubuhi na jioni, ndiyo
huwa napendelea kuichunguza timu hii, kwani huo ndiyo muda wa soka kwa
mwanasoka, muda anao amka na anao lala nilipenda kutambua na kujifunza
kutoka kwao. Nilikuwa na miaka 20 tu, na nilitamani kuwa mwanasoka kama
wao ( wale wa Simba) pia nilipenda kuwafuatilia sababu pia ni timu
niipendayo.
Lakini
kwa mara ya kwanza niliona kichefuchefu, nakumbuka kuna mwandishi mmoja
ambaye alikuwa akiandika katika magazeti ya BINGWA na DIMBA, na sasa
anaandika katika gazeti moja la michezo linalotoka mara mbili kwa wiki,
nikamtumia sms na kumwambia, " Kaka, huyu, daah! Nimemkuta (Jina la
mchezaji kapuni) katika uchochoro fulani hivi na ka- house girl, wa
nyumba ya mshkaji na kesho wanacheza mechi na Ashanti United ( wakati
ule wa ligi ndogo), hivi huwezi kuwaandika hawa, Kaka?" Sikuwahi
kujibiwa sms hii na hadi leo kalamu ya mwandishi huyu haijawahi kuandika
chochote kuhusiana na mambo kama haya.
Nilipopata
nafasi ya kushika kalamu nikasemea " Asante... Kuna siku nitaitumia
kalamu yangu kuandika mambo haya kwa uwazi na ukweli, na kamwe
haitamuhukumu Mwanasoka. Itamuhukumu ' hawala wa mchezo' ambaye amevamia
mchezo hasioufahamu miiko ya mchezo. Kwani Mwanasoka akiwa anatakiwa
kuwa mwadilifu wa kambi na ayefuata kanuni husika za klabu na miiko
muhimu ya kuzingatia ili kulinda kiwango chake kwa manufaa yake na klabu
yake. Lakini kwa Mwanasoka kamwe hataichukia kalamu hii zaidi ya
kuipenda na kuisifia, kwani itawaondoa ' mamluki wanaowatia nuksi'
katika malengo yao. Haya ndiyo madudu ya KLABU YA SIMBA SC ilipokuwa
Morogoro.
SIKU SITA ZA SIMBA MORO NA POINTI YAO MOJA: NA KOCHA MILOVAN
Simba ilifikia katika, Hotel ya
Usambara, ambayo humilikiwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Mzee Yusuph
Makamba. Kuna wachezaji waliolala katika vyumba vya gharama ya 20,000,
na wapo waliolala katika vile vya gharama ya 25, 000. Kocha Milovan
Curkovic, yeye aliandaliwa chumba cha gharama ya 50, 000. Vikaanza
vioja. Kocha akakataa kufikia Hotel isiyo na huduma ya Internet.
Viongozi kwa kushirikiana na Meneja wa Hotel hiyo wakamtafutia Kompyuta
yenye huduma ya Internet, lakini, Milovan, akakataa na kusema kwa
kiswahili kizuri 'Nataka yenye wireless' viongozi wachache tena wa ngazi
ya chini, wakashindwa na kuingia katika mtego wa Milovan, ambaye tangu
awali alionesha kutotaka kukaa katika Hotel ile. Golikipa wa makipa wa
timu hiyo akasema ' Hana lolote, hakuna cha Internet wala nini anataka
Mwanamke tu huyo kocha hamna kitu na sasa anaongea hadi Kiswahili...'
alikuwa akiongea mbele ya wachezaji wachache.
Milovan, akaamishiwa katika hotel yenye hadhi zaidi na gharama ya
chumba ni zaidi ya 60, 000. Hakwenda pamoja na timu akitokea hotelini.
Simba walitoka zao kivyao kutokea, Usambara, Milovan, akatokea ARC
Hotel. Wakapata pointi moja mbele ya Polisi Moro.
WACHEZAJI:
Walikuwa huru sana na walionekana kupitapita baadhi ya mitaa. Hawakuwa
na kiongozi imara. Na hata meneja, Nico Nyagawa, hakuweza hata kuwaonya
katika lugha ya mpira. Yote sababu Nyagawa naye anatambulika kama
mchezaji klabuni hapo na mkataba wake unamalizika punde na kuna timu
anakwenda kuichezea katika mzunguko wa pili wa ligi kuu msimu huu.
Angesema nini? Angemkanya nani? Tatizo la wachezaji likaanzia kutokuwa
na uongozi kambini, kocha yupo umbali kiasi na hata nahodha, Kaseja,
hayupo sawa kiutulivu, kuna mambo mabaya anayaona yakifanyika lakini
anatetea ajira yake. Unajua kwa nini alilia sana?
SIKU MBILI KABLA YA KUIVAA MTIBWA
Katika hotel, ambayo wachezaji walifikia, na kuwepo hapo chini ya
uongozi wa " Kishkaji na Majungu" wakaingia wapangaji wengine, walikuwa
kundi kubwa la wasichana zaidi ya 300. Pakawa hapotoshi. Wasichana hawa
ni wale wakaguzi wa vyuo vya juu. Nao wakapigwa na bumbuwazi, waliona
kama ndoto vile kukutana na mastaa wa soka nchini. Waliwaona, Mrisho
Ngassa na utitiri wa majina makubwa katika soka la nchi yetu.
Ukawa
mtihani mkubwa. Mwenye mbinu bora ndiye angeufaulu. Baadhi ya wasichana
wakaamua kubaki pale na kutandika vya kulalalia kwani, hotel zote za
jirani zilijaa. Mtego ukaanzia hapo. Na baadhi ya wasichana walifauru
vizuri, kwa sababu walikuwa na mbinu na maarifa zaidi ya baadhi ya
mastaa wa Simba. Wenye uchu na tamaa walinaswa kirahisi na wakachangia
asilimia 75 ya kipigo cha timu yao mbele ya Mtibwa.
KIGGY MAKASI NA WENZAKE NA KUNDI WA WAPENDA NGONO SIMBA
Katika miaka ya 90, timu ya Liverpool ilikuwa na
kikosi bora cha mchanganyiko wa wachezaji wazoefu na wale wenye umri
mdogo, na waliokuwa wakisifika kwa mchezo wa mzuri. David James, Robbie
Fowler, Jammie Reddknapp, Steve McManamann, Paul Ince, walikuwa
wachezaji bora katika soka la Uingereza, lakini hawakuwahi kupata
mafanikio yoyote hadi pale walipotawanyika katika timu hiyo. Chini ya
nyota hawa, Liverpool, ikaanza kupoteza makali uwanjani na kuwa
wapambaji wa magazeti, baada ya nyota hao niliowataja kuimarisha zaidi
jina lao la " Spice Boys" na kuwa maarufu na bora zaidi nje ya uwanja,
wakitumia muda mwingi kujirusha na kuiporomosha timu yao.
Wakati Kiggy Makasy akiwa bado anajiuguza, alikuwa mchezaji wa kwanza
wa Simba, kuwatia ' nuksi' alifanikiwa kumpata mwanachuo, mmoja ambaye
alikosa chumba na kwenda kulala naye. Sijui walichofanya, macho yangu
yaliishia hapo. Ghafla nikamuona Mrisho Ngassa, anashuka maeneo ya
jirani ambako kuna wanachuo walifikia alichelewa sana kurejea katika
chumba chake. Pia waliongiza wasichana katika vyumba vyao ni Nassoro
Chollo, ambaye alifungisha bao la pili kwa kupiga ' pasi mkaa' kwa, na
wengine ambao binafsi niliwaona ni, Ramadhan Chombo na mchezaji mmoja
hivi simtaji kwa heshima ya ndoa yake changa. Ilikuwa ni usiku wa
Jumamosi, kuamkia siku ya mchezo, Jumapili na wakachezea za kutosha tu,
pale, Jamhuri. Chollo, Ngassa, Redondo, wote waliwekwa nje katika
kipindi cha kwanza. Na hata, walipoingia walifanya nini? Chollo kumtoa
machozi Kaseja, kwani hakuwa fiti kabisa na kama angekuwa fiti angesogea
na mpira mbele lakini alilala na msichana akawa na uchovu, taabu ya
nini? Akachoma, lango lake.
JUMA KASEJA
Kwa kipindi chote tangu naanza
kumfahamu miaka kumi, iliyopita, nimegundua, tabia nyingi za ajabu
kuhusu, nahodha huyu wa Simba na Taifa Stars. Ni msiri sana, mcheshi,
mwenye kupenda ushirikiano, anayejituma, mwenye hitaji la ushindi katika
moyo wake. Lakini, kama mwanadamu mwingine, Kaseja, naye ana wivu. Wivu
wa kufanikiwa na kuendelea kuwa juu. Nadhani vitu hivi ndivyo
vilivyomsaidia sana kuwa miongoni mwa makipa bora kuwahi kutokea nchini.
Atakumbukwa kwa mengi sana mazuri, ambayo ameyafanya katika wakati wake
na hadi sasa bado namtambulisha kama ' Hasiyegusika wala kufananishwa"
Nani kama yeye? Nani anayekuja kuvaa ' glovu' zake? Hakuna, hilo ndiyo
jibu sahihi. Kwa muda wote wa uwepo wa timu pale hotelin, Kaseja aliweka
akili yake katika michezo miwili ya timu yake dhidi ya Polisi Moro na
Mtibwa, alikuwa muda mwingi mwenye kuswali.
SHOMARI KAPOMBE:
" Masikini, Kapombe, amegombana na
Kaburu, hadharani vile... Sijui maisha yake yatakuwaje, Simba?" Ni
maneno ya mwanachama mwandamizi wa Simba, akizungumzia kitendo cha
mlinzi kinda wa timu hiyoa Kapombe, kurushiana maneno makali na Makamu
Mwenyekiti wa klabu yake, Geofrey Nyange Kaburu, ambaye alikuwa
akimshutumu Kapombe kama sehemu ya kufungwa kwa timu yao na Mtibwa
Sugar. Awali wakati mchezo ukienda mapumziko, Kapombe alionekana kuanza
kumrushia maneno makali ya kumshutuma Felix Sunzu. Kabla ya Sunzu,
kuanza kumjibu, lakini haraka, Kaseja, akawatuliza.
Wakati wakiwa,
hotelin, mlinzi wa kimataifa kutoka Kenya, Paschal Ochieng, alikuwa
akiwaambia, Amir Maftah na Kapombe, kuwa wawe makini, kwani ndiyo
waliochangia, Polisi Moro, kupata, bao wakati wa mchezo baina yao. Akawa
anawaelekeza maeneo ambayo walitakiwa kuwepo, alimwambia, Maftah, kuwa
alipitika kirahisi na kuruhusu, krosi ambayo ilizaa bao pekee la Polisi,
na akamwambia, Kapombe, kuwa hakuwa katika eneo sahihi kama mlinzi wa
kati. Kapombe, akamjibu ' hata wewe hukuwa katika eneo lako'. Dogo, huyu
hivi ameota ' majipu kwenye kwapa zake' naye ' hagusiki' kwa mpira
gani? Ule wa kukimbizwa na ' Babu, Kisiga?' chunguza vizuri sababu ya
mabao waliyofungwa Simba na Polisi kisha Mtibwa Sugar, utagundua kuwa
Kapombe hagusiki Simba.
MSIKILIZE OBADIA MUNGUSA ANAVYOMZUNGUMZIA KABURU
" Unajua hivi sasa sipo na timu, kuna
mambo hayapo sawa kati yangu na Bosi, Kaburu. Unajua yeye ndiye
aliyenisainisha mkataba wakati nasajiliwa na Simba, hivyo kila kitu
ananisimamia yeye" anasema mlinzi huyo ambaye hayupo kikosini hivi sasa.
' Unajua wakati wananisajili kuna makubaliano ambayo kimsingi pande
zote zilitakiwa kuyatekeleza, lakini haikuwa hivyo. Ndipo nikajaribu
kuulizia mbona makubaliano wanayakiuka na wala hayakuwa kama hali
ilivyokuwa, Ikawa, kosa, kwanza alinionesha dhaharu kubwa sana, pia
aliniambia wazi naweza kuondoka, kwani sina nafasi ya kucheza.
Akaniambia wewe tafuta tu timu, Simba huna nafasi. Sikuwa na jinsi
nikatafuta timu nyingine, lakini kuna wachezaji wanaonekana wana thamani
zaidi ya wengine kikosini, labda hiyo ndiyo sababu ya wachezaji wengine
kudharaulika. Ukitazama aliwaleta wachezaji kama Kanu Mbiyavanga, Linno
Musombo na Mussa Mudde baada ya kuwapatia pesa nyingi, lakini walifanya
nini walipokuja? Kwa nini pesa kama ile tusipewe wazawa? Kwani hao
wageni hawana jipya lolote"
"
Unajua nimerudishwa sana nyuma kwa kipindi ambacho nimekuwa, Simba,
lakini nimejifunza mambo mengi sana kama mchezaji wa soka. Lakini
nitabaki namshangaa, Kaburu kuanzia namna anavyoyachukulia matatizo ya
wanadamu wenzake hadi katika uongozi wake wa soka. Unajua usajili
anafanya yeye, si mbaya lakini amekuwa akikurupuka sana kwani akiambiwa
mahali fulani kuna mchezaji anakwenda na kumsajili, na ndiye aliyewaleta
kina, Ochieng baada ya kina Musombo kuonekana si wachezaji wazuri, pia
amekuwa akiingilia hadi mambo ya utawala wa benchi la ufundi, sasa
unabaki unajiuliza huyu ni kiongozi wa soka kweli?"
Je, kama mambo yatawekwa sawa na kupewa anachodai, Mungusa anaweza kurejea katika timu hiyo?
" Nina uchungu sana na kilichonitokea katika klabu hiyo ( Simba) kwanza
mtu unakuwa na majeraha ya mara kwa mara tena yasiyoeleweka, halafu
unakuta tena kwenye malipo wanakuzingua, mimi nina majukumu yangu pia.
Kuna viongozi wamekuwa wakinipigia simu na kuniambia nirejee kikosini na
nijishushe kwa Kaburu, kwa madai kuwa ndiyo tabia yake. Lakini sidhani
mana nina hasira nao sana"
" Kwa mfano mechi ya juzi hadi yule mtoto
kacheza! Simba ndiyo imekuwa hivyo sasa?" anahoji mlinzi huyo mwenye
miaka 24. " Kama ipo ipo tu, nasubiri dirisha dogo kujua nini kitatokea"
OKWI NAYE NI TATIZO KUBWA SIMBA SC
Ni mchezaji mzuri sana na anajitolea
kwa timu yake, lakini ni kama kila mtu ndani ya timu hiyo ameekeza
nguvu zake kwa Mganda huyu kitu ambacho ni hatari. Kuna tetesi za
chinichini kuwa baadhi ya wachezaji wazawa wamekuwa wakichukia kuona
Okwi anavyotazamwa zaidi ndani ya timu hiyo kuliko wachezaji wengine. Ni
lazima timu itazame upya namna ya kucheza michezo mfumu bila Okwi kwani
tayari wapinzani wengi wamekuwa wakimuandalia mikakati ya kumzima na
sasa wameanza kupata dawa yake. Amewaambia wapenzi na mashabiki wa timu
hiyo kuhama na kutafuta timu nyingine ya kushangilia kama wanaumizwa
zaidi kuliko wao na matokeo ya timu hiyo hivi sasa. Hi ni kauli ya
mwisho inayoweza kuthibitisa kuwa hivi sasa yeye ndiye staa zaidi
kikosini. Ameingia katika mzozo mkubwa na wachezaji wazawa kwa sababu ya
dharau zake.
MENEJA/ MISHAHARA YA MAPROO
Simba inatakiwa kuwa na meneja imara na
mwenye kuripoti taarifa za siri kwa uongozi kuhusiana na wachezaji
ambao hukiuka miiko ya kambi na kuchangia matokeo mabaya uwanjani.
Nyagawa hawezi jukumu hili. Mishahara ya wachezaji wengi wa kigeni ndani
ya timu hiyo kwa miaka ya karibuni imekuwa ghali sana, na hilo
limepelekea sononeko lisilokwisha kutoka kwa wachezaji wengi wazawa,
ambao hulipwa mishahara kiduchu, wale wazawa wanaoona wenzao
wanapendelewa mno wakati hawatoi matunda mazuri uwanjani. Nalo hili
litazamwe.
No comments:
Post a Comment