Washiriki walioingia fainali hizo na kujikuta wakiwa katika kimbembe cha kuwania Sh milioni 50 na mkataba wa kurekodi nyimbo zao lililotolewa na Kampuni ya Zantel ni Nshoma Ng’hangasamala (EBSS07), Walter Chilambo (EBSS12), Wababa Mtuka (EBSS11), Nsami Nkwabi (EBSS06) na Salma Abushiri (EBSS09).
Mtanange huo utasindikizwa na wasanii mbalimbali maarufu kama vile Rich Mavoko, Ommy Dimpoz, Ben Pol, Linah, Amini, Mzee Yusuf, Haji Ramadhan, Mwasiti, Ditto, Laila Rashid, Linex na Barnaba.
Akizungumzia shindano hilo, jaji mkuu wa EBSS 2012, Ritha Paulsen, alisema maandalizi ya fainali yamekamilika, na kuwaomba Watanzania wengi wajitokeze kutazama fainali hizo katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
“Pamoja na washiriki kutoa burudani kali siku hiyo, pia tumewandalia burudani nyingine nyingi na za kipekee, hii yote ni kuwaonyesha kuwa shindano hili ni zaidi ya mashindano bali ni burudani pia,” alisema Paulsen.
Akizungumzia zaidi fainali hizo, alisema shindano bado halijafungwa kwani wapenzi wa shindano hilo wanatakiwa kuendelea kumpigia kura mshiriki wanayempenda ili aibuke mshindi.
No comments:
Post a Comment